Ndolanga |
Mjumbe wa Heshima wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Muhidin Ndolanga amelitupia lawama shirikisho hilo, akisema linahusika moja kwa moja ‘kutengeneza’ mgogoro alioutafsiri kuwa una dhamira ya masilahi binafsi kwa baadhi ya watu, hatua iliyopelekea kukwaruzana na serikali.
Aidha, amesema uamuzi wa serikali kuingilia kati utendaji wa shirikisho hilo ni sahihi kwa vile kinachoendelea ndani ya TFF, siyo tu kwamba hakikubali, bali pia hakivumili na wadau wengi wa soka. Akizungumza na gazeti hili jana, Ndolanga alisema taswira ya sasa TFF, ni uroho wa madaraka kwa baadhi ya watu ambao hawako tayari kuona mabadiliko makubwa yanafanyika.
Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), tayari limeshaonya kuwa Tanzania inaweza kufungiwa iwapo itabainika kuwa serikali inaingilia kati utendaji wa TFF.
“Fifa haiwezi kutoa onyo bila TFF kulalamika. Kuna mtu amepeleka taarifa Fifa. Ndani ya TFF kuna watu wanafanya kazi kwa woga. Kama ningekuwa mimi (Ndolanga), ningesema wazi nahusika kuwajulisha Fifa na ningetoa sababu.
Aliongeza: “Binafsi sioni mahali serikali ilipofanya makosa mpaka sasa. Ingefanya makosa mimi siogopi lazima ningeikosoa, ningesema hili hapana---mmekosea.
Muda wa kukaa madarakani kwa Tenga na timu yake umekwisha, walitakiwa wapangilie mambo yao mapema ikifika Desemba 31 waondoke waache uongozi mpya.”
Muda wa kukaa madarakani kwa Tenga na timu yake umekwisha, walitakiwa wapangilie mambo yao mapema ikifika Desemba 31 waondoke waache uongozi mpya.”
Kauli ya Ndolanga imekuja siku chache baada TFF kupitia kwa Ofisa Habari, Boniface Wambura kusema kuwa Fifa wamewasilisha barua ya kuionya Tanzania kuwapo na uwezekano wa kufungiwa kuitokana na serikali imeingilia uhuru wa taasisi hiyo.
Wambura alisema pia Fifa inachunguza suala hilo na itakapobainika kuwa Serikali imeingilia kati, basi kuna uwezekano mkubwa kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa.
Wambura alisema pia Fifa inachunguza suala hilo na itakapobainika kuwa Serikali imeingilia kati, basi kuna uwezekano mkubwa kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa.
Serikali iliingilia kati mchakato mzima wa uchaguzi wa TFF, ikitaka kuitishwa mkutano mkuu wa marekebisho ya katiba na kisha mkutano mkuu wa uchaguzi, mambo yote hayo kufanywa ndani ya siku 80.
Kuhusu marekebisho ya katiba ambayo TFF walidai ndiyo yaliyosababisha kuchelewa kufanya uchaguzi wao baada ya kuambiwa na Fifa kuingiza kipengele cha leseni za klabu na kushauri kuundwa kwa Kamati ya Rufaa.
Ndolanga alisema: “Suala la marekebisho wanayotuambia, mnadhani nchi zote za Afrika zimeshafanya au ni hawa TFF tu wanataka kutupeleka puta? Kwanza hailazimishwi kufanya marekebisho papo kwa hapo.
“TFF walikuwa na uwezo wa kufanya uchaguzi na kuwaandikia barua CAF na FIFA, kuwa wamefanya uchaguzi na marekebisho yote ya katiba waliyoagiza wanayakasimisha kwa uongozi mpya.”
Alisema hali hii ikiachwa iendelee ndani ya TFF, wanachama wao watachoshwa na kuna uwezekano siku moja wakaamua kujiorodhesha na kufanya mkutano kwa mujibu wa kolamu yao na utakuwa halali, na katika mkutano lolote linaweza kutokea.
chanzo gazeti la Mwananchi
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa