jamaa karudi usiku wa manane. Moja kwa moja akazama chumbani, akafunua blanketi, akaiona miguu minne badala ya miwili aliyozoea. Jamaa akafunika blanketi taaratibu, akachukua bonge la rungu, akaitwanga ile miguu kwa nguvu zote halafu akaelekea sebuleni kutuliza hasira. Kutahamaki akamkuta mkewe amejipumzisha sebuleni. Mkewe akamwambia: Wazazi wako wamekuja leo kututembelea, nimewaachia
chumba chetu walale
_____________________________________
Wavuta bangi wawili walionna embe juu ya mti, wakaamua kulitungua . Walirusha mawe mengi lakini hawakufanikiwa kuliangusha. Mvuta bangi mmoja akasema isije ikawa embe lenyewe bichi, ngoja nipande juu nikalicheki. Baada ya dakika kadhaa yule mvuta bangi akashuka chini akamwambia mwenzake "nimelibonyeza limeiva vizuri kabisa, tuendelee kulitungua mwanangu
3 comments :
hii kali si angechuma tu hilo embe alivyopanda kuangalia kama limeiva au laaah !!!!!!
hah hah hh ah ah ahah ah ah ahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
kicheko gani iko ?
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa