Translate in your language

Thursday, January 31, 2013

MOTO WATEKETEZA KIWANDA CHA CHEMICOX

Moto mkubwa umekiunguza Kiwanda cha vipodozi Chemi Cotex kilichopo Africana, maeneo ya Mbezi Beach, Dar es Salaam na kukiteketeza katika muda wa takriban dakika 45


Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. kwa mujibu wa Issa Michuzi blog, inahisiwa chanzo inawezekana kuwa ni hitilafu iliyotokana na fundi aliyekua akichomelea (welding) kitu ndani ya kiwanda hicho.
 moshi mkubwa ukitanda katika anga ya kiwanda hicho 
 wafanyakazi wakiwa nje ya kiwanda hiko baada ya kunusurika na kutoka kiwandani 

Taarifa zinasema kuwa baadhi ya watu walianza kuyarushia mawe magari ya kikosi cha zima moto yalipowasili katika eneo la tukio kiasi cha tkutishia usalama was watu wengine. Habari zaidi zitaletwa baada ya kupatikana.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)