Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk
Harrison Mwakyembe, katikati ya mwaka huu kuahidi kuanzisha usafiri huo kati ya
Stesheni na Ubungo Maziwa kwa uapande
reli Kati inayotumiwa na kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kati ya Kurasini na Pugu Mwakanga kwa ile ya Shirika
la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara).
Tangu Dk Mwakyembe atoe kauli hiyo tumeshuhudia marekebisho na ukarabati wa
miundombinu umekuwa ukifanyika katika
njia hizo za reli.
Ziara iliyofanywa na Kamati ya Bunge pamoja na uongozi wa
Mkoa wa Dar es Salaam chini ya RC Said Meck Sadiq katika njia hizo ikiwamo ya
umeonyesha kuwa, matayatisho yamekamilika.
Tunawapongeza wote ambao kwa njia moja, au nyingine wameshiriki kufanikisha mpango huo
unafanikiwa kama ilivyopangwa.
Hadi mwisho wa wiki
hii mpango huo ulikuwa umefikia hatua ya wadau wa sekta hiyo kujadili kiwango
cha nauli ikipendekezwa kuwa iwe Sh800 kwa abiria wa njia ya reli ya kati na
700 kwa ile ya Tazara na Sh100 kwa wanafunzi.
Tunaamini kuwa suala la kiwango cha nauli, ubora wa huduma
ambazo zitatolewa katika treni hizi kwa abiria, pia nalo halina budi kuangaliwa
kwa umakini mkubwa ili kutowaumiza watumiaji wake.
Tunashauri kwamba wote waliotakiwa kuondosha nyumba, au
vibanda vyao vya biashara kando ya njia hizo za reli wafanye hivyo haraka ili
kuepusha kutokea ajali na madhara mengine kwao na watumiaji wengine wa huduma
hiyo.
Tunasema hatua iliyofikiwa kuelekea kuanza kwa safari hizo
itaendelezwa ili hatimaye usafiri huo uanze na hivyo kusaidia kuondoa kero na
tatizo sugu la msongamano wa magari na abiria jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, tunatoa angalizo kuhusu usimamizi na uendeshaji
bora na mzuri wa usafiri huo ambao utafanywa na TRL na Tazara ambao nui
wazoefu.
Kwa maana hiyo, tunadhani kuwa miradi hii itakuwa endelevu
ikiachwa ijiendeshe bila kuingiliwa na wakubwa au watu wenye ushawishi katika
jamii, au kugeuzwa kitegauchumi cha wachache watakaonufaika na mapato
yatakayotokana na utoaji wa huduma hiyo.
Angalizo jingine tunalitoa kwa watu wenye uwezo kifedha na ambao wamekuwa
wakiingia katikati ya Jiji kwa magari yao binafsi, wasifanye hiyo badala
yake watume usafiri wa treni hizo ili
kupunguza foleni.
Hata hivyo, tunashauri mamlaka zilizopo ziangalie suala la
maegesho ya magari na ulinzi katika eneo
la Ubungo ili kuwawezesha watu wengi kukubali kuacha magari yao na kupanda
treni.
Hili, tunaamini likifanyika, msongamano sugu wa magari
katika barabara zetu utakuwa umepata dawa ya kudumu.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa