Translate in your language

Wednesday, August 15, 2012

Tanzania na Mpango wa kupunguza Foleni Dar Es salaam

mafundi wakiendelea na kazi katika moja ya barabara za mjini
Dar es salaam 
Watanzania wamepokea mpango wa serikali wa kuanza rasmi miradi ya kuondoa msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, ambayo kwa mujibu wa utafiti wa serikali utagharimu shilingi bilioni 4 (dola za Kimarekani 2.5) kila siku.

Kwa miaka 20 iliyopita, serikali imekuwa ikijadili upanuzi wa mtandao wa barabara jijini Dar es Salaam na mfumo wa reli , lakini hatimaye imeidhinisha mpango wenyewe mwezi Julai mwaka huu.

Awamu ya kwanza ya mradi huu itajumuisha ujenzi wa vituo vya mabasi 29 na barabara ya basi ya kilometa 21 tu kutoka Kimara hadi Kivukoni jijini Dar es Salaam, kuhudumia wasafiri wa magari 400,000, kwa mujibu wa Cosmas Tekule, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka jijini Dar es Salaam.

Mradi huu utagawanywa katika awamu sita na unakadiriwa kutoa ajira 80,000, Tekule aliiambia Sabahi.

Awamu ya kwanza ya ujenzi- kutoka Kimara kwenda katikati ya mji- utakamilika mwezi wa Disemba, alisema. Barabara nyingine zitaongezwa katika awamu inayofuata kwenye barabatra ya Ali Hassan Mwinyi, Kilwa, Nyerere, Mandela na Bagamoyo, ambazo ni barabara kuu zinazoingia katikati ya mji. Mradi wote huu unatarajiwa kukamilika mwaka 2005, kwa mujibu wa Tekule.

Mara utakapomalizika, mabasi madogo ya kusafirisha abiria, yanayojulikana kama "daladala", yataondolewa katikati ya mji na mabasi mapya yenye uwezo wa kubeba abiria 150 yataanzishwa, Tekule alisema.

Abbas Malibiche, mwenye umri wa miaka 46, dereva wa basi jijini Dar es Salaam, alisema ingawa madereva wa daladala wanatarajiwa kupoteza kazi zao kutokana na mradi mpya, msongamano kwa sasa hauvumiliki.

"Siku hizi hatupati pesa. Tunamaliza mafuta kwenye foleni zisizoisha. Inachukua saa tatu kusafiri umbali wa kilometa 20...nafikiri mradi huu mpya ni mzuri kwa uchumi," Malibiche aliiambia Sabahi.


Waziri wa Usafiri Harrison Mwakyembe aliiambia Sabahi kwamba wazo la kuanzisha njia maalumu kwa mabasi jijini Dar es Salaam lilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1992 na Rais Ali Hassan Mwinyi.

"Hapo nyuma, tatizo la foleni halikuwa kubwa kama tunalokabiliana nalo sasa. Rais Mwinyi alisema Dar es Salaam ilikuwa inakua haraka sana na inahitaji mfumo wa usafiri wa uhakika," aliiambia Sabahi.

Alisema awamu ya kwanza itagharimu dola milioni 274, ikigharimiwa na serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia.

Mwakyembe alisema mradi wa wizara kugeuza reli ya mizigo kuwa mfumo wa reli ya kutoa huduma katika vitongoji jijini utakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Septemba.

"Ukarabati wa mfumo wa reli wa zamani ulioachwa na wakoloni unaendelea na tumenunua mabehewa mapya na vichwa vya garimoshi," Mwakyembe aliiambia Sabahi. "Tunataka kumaliza kabisa tatizo la foleni la magari Dar es Salaam ambalo linaigharimu sana serikali."

Katika mpango huo, treni za kusafirisha watu mjini zitafanya kazi kati ya Ubungo na katikati ya jiji, wakati idadi ya barabara za pembezoni zitawekwa lami ili zipitike wakati wote.

Juliet Antipas, mwenye umri wa miaka 38, mkaazi wa Dar es Salaam, aliusifu mradi mpya wa serikali, akisema utawasaidia watu kufika kazini haraka. "Tunapoteza muda mwingi katika foleni barabarani, muda ambao ungeweza kutumika kuzalisha zaidi na zaidi," Antipas aliiambia Sabahi.

Zaidi ya shilingi bilioni 4 kupotea kila siku kwa sababu ya foleni za barabarani
Waziri wa Ujenzi John Magufuli alisema umuhimu wa mradi hauwezi kusisitizwa zaidi.

"Dar es Salaam inachangia karibia asilimia 80 ya pato la taifa," Magufuli aliiambia Sabahi. "Watu wanapoteza muda katika foleni za barabarani. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kwamba foleni zinaugharimu uchumi zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 4 kwa siku."

Alisema baadhi ya wafanyakazi wanatumia saa nne hadi sita kwenda na kurudi kazini kila siku.

Magufuli alisema mradi wa serikali ni pamoja na ujenzi wa barabara za magari yaendayo kasi ili kupunguza muda unaotumika katika taa za kuongozea magari. Barabara ya kwanza ya magari yaendayo kasi itajengwa katika makutano ya TAZARA ambapo barabara ya Nyerere kuelekea Uwanja wa Ndege na Barabara ya Mandela kuelekea Uwanja wa Ndege zinakutana.

Hii itapunguza foleni za barabarani wakati wa saa za msongamano kuanzia masaa manne mpaka takriban dakika kumi na wafanyakazi watakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi kwa muda uliookolewa, alisema Magufuli.

Finnegan Kato, mwenye umri wa miaka 51, mfanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam anayeishi katika Kitongoji cha Kibamba, alisema ana furaha kwamba mradi wa magari yaendayo kasi hatimaye umeanza.

"Fikiria: Ninatakiwa kuamka saa 10:30 alfajiri kujiandaa kwa ajili ya kuwa barabarani saa 11:15 na kusafiri kwa kilometa kama 30 kutoka nyumbani hadi kazini kwangu," Kako aliiambia Sabahi. "Kwa kawaida, ninatumia dakika 20 barabarani, lakini kama nikishindwa kutoka muda huo na kuwasha gari langu saa 12:00 asubuhi, na hizi kilometa 30 kwa kawaida ninafika ofisini baada ya saa 3:00 asubuhi."

"Kama kuna kitu kizuri ambacho serikali imefanya, basi ni hiki," alisema.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)