Translate in your language
Tuesday, August 14, 2012
Helikopta tatu za Uganda zikiwa njiani kuelekea Somalia zimepotea katika ardhi ya Kenya. Maafisa wa jeshi la Kenya wamesema leo kwamba helikopta nne ziliondoka Uganda na moja ikatuwa mjini Garissa
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Kenya Bogita Ongeri, helikopta hizo zilipotea karibu na eneo la mlima Kenya, lakini rubani mmoja aliweza kuwasiliana nao, akiomba msaada.Kwa mujibu wa msemaji huyo, mvua na hali mbaya ya hewa zilihujumu juhudi za uokozi na Ongeri akaongeza kwamba kundi la waokowaji limepelekwa sehemu hiyo ya ajali. Hata hivyo alisema hawafahamu kwa uhakika ni wapi hasa ajali hiyo ilitokea kwa sababu bado hali ya hewa ni mbaya. Helikopta hizo aina ya Mi-24 zinauwezo wa kubeba hadi abiria wanane.
Helikopta hizo ambazo ziliondoka Uganda jana, zinahofiwa kuwa zimeanguka kwenye eneo moja la milima lililojaa misitu, karibu na mlima wenye theluji wa Kenya na ambao una urefu wa mita 5,199. Mkuu wa Polisi wa mkoa Francis Munyambu amesema taarifa walizonazo ni kwamba kuna mahala mahsusi ambapo inaaminiwa ndiko kulikotokea ajali hiyo.Aidha Mbali na helikopta za kivita M-24 Uganda inaripotiwa pia kupeleka Somali ndege za uchukuzi zilizotengenezwa Urusi aina ya Mi-17.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa