Waokoaji waligundua mabaki ya helikopta mbili za Uganda zilizokuwa zimepotea karibu na Mlima Kenya hapo Jumanne (tarehe 14 Agosti), huku wanajeshi wawili wa Uganda wakifariki dunia na angalau watano wakipatikana hai, liliripoti shirika la habari la AFP.
"Habari njema ni kwamba tumeweza kuwapata manusura watano na hivi punde wamesafirishwa kwa ndege kuelekea kwenye usalama," alisema Simon Gitau, muhudumu wa ngazi za juu katika Idara ya Wanyamapori ya Kenya, ambayo ilihusika na uokozi. "Wana hali nzuri baada ya kusogea mbali kando ya eneo la ajali."
Mkuu wa Jeshi la Kenya, Jenerali Julius Karangi, aliwaambia waandishi wa habari kwamba moja kati ya helikopta hizo mbili "ilipatikana ikiwa imeungua yote, na nyingine ikining'inia kwenye mlima". Bado watu saba hawajulikani walipo.
Helikopta nne ziliondoka Uganda siku ya Jumapili kwa ajili ya kuelekea mji wa bandari wa Somalia, Kismayo, kuvisaidia vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia katika operesheni yake ya kijeshi dhidi ya al-Shabaab.
Moja kati ya helikopta nyengine mbili iliwasili Garissa kama ilivyopangiwa kwa ajili ya kuwekewa mafuta, na nyingine ilitua kwa dharura kwenye Mlima Kenya na kupiga simu ya redio kuomba msaada. Wanatimu wake saba wako salama na imeshaokolewa.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa