Translate in your language

Friday, August 10, 2012

PROFESA MAHALU ASHINDA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI

Wanahabari wakimzonga Profesa Mahalu (katikati)
 baada ya kushinda kesi yake leo katika Mahakama ya
 Hakimu Mkazi Kisutu.

ALIYEKUWA Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili  baada ya kuonekana ushahidi uliotolewa na upande wa walalamikaji kutojitosheleza.

Akisoma hukumu hiyo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hakimu Ilvine Mugeta, alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili amebaini kuwa Profesa Mahalu  na  aliyekuwa Mkuu wa Fedha na Utawala katika ubalozi huo, Grace Martin, hawana hatia na hivyo kuwaachia huru.

Hakimu Mugeta alisema kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa walalamikaji unajichanganya na kuonekana wazi kuwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili Profesa Mahalu si za kweli.

Prof. Mahalu aliyekuwa anatetewa na wakili mkongwe Mabere Marando na wenzake. kwa taarifa zaidi bonyeza hapa 

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)