Translate in your language

Thursday, August 9, 2012

UMEPATA SIKIA AU ONA HII?


MUUZA MKAA ABEBA MAITI YA MKE WAKE KATIKA BAISKELI KUTOKANA NA HALI NGUMU YA MAISHA

,Jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Athumani Juma mkazi wa mtaa wa juhudi zako kata ya mwembesongo mkoani Moro,anayefanya shughuli za kuchoma mkaa katika kijiji cha Maji chumvi Wilaya ya Mbvomero amepata mkasa mzito wa kufiwa na mkewe kwenye kijiji hicho na kuradhimika kusafirisha mwili huo kwa kutumia usafiri wa baiskeli kutoka kijiji hicho hadi Moro mjin ikiwa ni umbali wa takribani kilomita 25 baada ya kukosa fedha ya kukodi gari.


Athuman ambaye aliupakia mwili huo kwa umahiri mkubwa kwa kutumia miti na viloba akijalibu kuuficha akihofia kutogundulika na wanausalama
,
Hata hivyo kutokana na safari ndefu iliyokuwa na changamoto nyingi zikiwemo za kunyeshewa na mvua ambapo alipofika maeneo ya kihonda baadhi ya watu waligundua na kuamu kumjulisha mwandishi wa habari hizi ambapo nilimfuatilia ambapo nilifanikiwa kukutana naye maeneo ya Msavu na kwamba baada ya kuona na mpiga picha aliingiwa na hofu kubwa akitaka kukimbia.

Hata hivyo nilitumia busara nyingi za kumtuliza sambamba na kumpa pole baada ya kuwa katika hali yake ya kawaida nilimhoji kuhusiana na mkasa huo ambapo alidai kwamba yeye na mkewe wanaishi mtaa wa juhudi zako na kwamba kwa pamoja wanafanya kazi ya kuchoma mkaa kwenye msitu wa kijiji cha Maji chumvi.

"Tuhapokwenda kwenye kazi hiyo ya mkaa huwa tunakaa huko zaidi ya siku tatu hivyo tukiwa huko usiku mke wangu ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo kwa kipindi kirefu alikufa ghafla usingizini,nimeamu kuja mjini kukodi gari la kuludisha mwili jamaa wanataka lakini moja kubeba maiti mimi nilikuwa na elfu 40 wamekataa nikaona mwili wa mke wangu unaweza kuozea ndani ndipo nilipojifunga kibwembwe na kuusafirisha kwa kutumia baiskeli"alisema kwa Uchungu Bw Athuman ambaye ameachiwa watoto wawili na marehemu w2a mwishon akiwa na umri wa mwaka mmoja.


Aidha Athumani ameongeza kusema kwamba kwenye kibanda chao cha huko Maji Chumvi aliacha vitu mbambli mbali hivyo baada ya kufanikiwa kuuludisha mwili wa mkewe nyumbani kesho yake alikuwa na safari ya kuludisha mizigo iliyopo kwenye kibanda hicho ambacho hakina mlango.

Mwandishi wa habari hizi aliguswa na jambo hilo hivyo aliamu kutumia usafiri wake wa pikipiki na kwenda kwenye kijiji hicho kuludisha mizigo ya marehemu pamoja na watoto ambao aliwahifadhi kwa majirani

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)