Translate in your language

Saturday, March 20, 2010

SIMBA YAREJEA KWA KISHINDO BONGO

 

SIMBA YAREJEA KWA KISHINDO BONGO

 

 

Na Mwanablog wetu Dar

 

MSAFARA wa timu ya Simba ulirejea nchini jana asubuhi ukitokea nchini Zimbabwe ambako juzi ilivuna ushindi wa mabao 3-0 huku Kocha Mkuu wake, Patrick Phiri, akienda kwao Zambia kusalimia.

Simba imerejea ikiwa ni siku moja tu baada ya kutoa kipigo hicho kwa timu ya Lengthens kwenye mechi ya  michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (Caf), iliyopigwa kwenye Uwanja wa Rufaro, mjini Harare.

Kwa mujibu wa Meneja wa Simba, Innocent Njovu,  Phiri amekwenda Zambia kwa mapumziko mafupi na atarejea kesho kwa ajili ya kuiandaa timu hiyo kwa mechi yao ya marudiano dhidi ya Lengthens na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kuhusu michuano ya kimataifa, Njovu alisema lengo la Phiri si kuiandaa timu kushinda katika mechi ijayo tu dhidi ya Wazimbabwe, bali pia ni kuandaa Simba bora kwa msimu ujao.

Alisema malengo ya kocha huyo na uongozi, ni kurejesha makali ya timu hiyo kwenye michuano ya kimataifa kama ilivyowahi kufanya mwana 2003 ambapo Simba ilitinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikiwa chini ya Kocha Mkenya, James Siang'a, Simba ilifika hatua hiyo baada ya kuing'oa Zamalek ya Misri iliyokuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo yenye utajiri mkubwa.

Naye Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, alisema kuwa mechi ilikuwa ngumu na licha ya kuwafunga hawatabweteka na ushindi huo.

Kipa namba moja wa timu hiyo, Juma Kaseja, alisema ushindi walioupata umechangiwa na maandalizi mazuri waliyoyafanya na kusema kitu muhimu kwao ni kuzidi kujifua zaidi.

Wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko mafupi kabla ya kuripoti kambini hapo keshokutwa tayari kujiandaa na mechi ya marudiano wiki mbili zijazo.

 

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)