Sunday, May 27, 2012

TULIPO KWA SASA !!!!!!!


NDEFU NDIO, LAKINI JITAIDI UISOME HII NAKALA


Na Stella Aron

NI miaka mingi sasa tangu kupata uhuru, kumekuwa na harakati mbalimbali za kuwawezesha wananchi kutambua ama kushiriki mambo mbalimbali ya kuboresha maisha ya jamii.

Serikali na asasi zisizo za kiserikali zimeshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuendesha harakati hizo.

Pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kuhamasisha wananchi, bado kuna mambo mengi  ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi zaidi hasa katika kipindi hiki cha utandawazi pamoja na kukabiliana na mfumo wa soko huria.



Thursday, May 24, 2012

TASWIRA YETU !!!!!!



Baadhi ya wafanyabiashara wa maji wakiwa kwenye foleni hali hiyo imekuwa ikiyakumba maeneo mengi kwa ukosefu wa maji na kulazimika kununua dumu moja kwa bei kati ya sh. 400 hadi 1000

Mnyika ashinda kesi kwa mara nyingine tena


Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika (Chadema)  amemshinda tena Hawa Ng'humbi (CCM) baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kutoa hukumu  kuwa ushindi wa Mbunge Mnyika  uliofanyika Oktoba 31, 2010 ulikuwa wa halali

Saturday, May 19, 2012

ETI!!!!!! KUTEMWA UWAZIRI: Maige afichua siri *Mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *Kuanika uozo wa Maliasili bungeni

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.
Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.
Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.

Tuesday, May 15, 2012

AAAAH KAZI KWELI !!!!!!!!

lakini kweli banaaa!!!!!! Adui yako mwombee njaaa