Uongozi kuogelea bado waogopwa Na Mwanablog wetu UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), ukizidi kukaribia kasi ya uchukuaji fomu za kugombea ya wadau wa michezo bado si ya kuridhisha. Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Ofisa Michezo Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohammed Kiganja, alisema kuwa hadi sasa ni wagombea saba waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho. Kiganja alisema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Aprili 3, ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kugombea ni Aprili mosi. Alisema, awali uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika Machi 27, lakini uliahirishwa kutokana na wagombea kutojitokeza. Kiganja aliwataja wagombea waliojitokeza kuwa ni Alex Mosha anayegombea nafasi ya Rais; Noel Kihunsi anayetetea ukatibu mkuu; Ramadhani Namkoveka aliyejitosa kwenye ukatibu msaidizi na uenyekiti wa kamati ya ufundi. Wengine ni Ayoub Andrew, anayetaka uhazini msaidizi, Kalufya Baneti, anayegombea kamisheni ya wachezaji na Mamboleo Gregory ambaye hajaainisha nafasi anayowania. Kiganja alitoa wito kwa wanamichezo mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali ili kulisukuma mbele gurudumu la maendelea la mchezo huo, ambapo fomu zinapatikana ofisi za BMT. |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa