KAMPUNI ya Multchoice Tanzania, Multchoice Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imezindua rasmi huduma zake za Dstv zitakazo kuwa zikitumika kutolea mafunzo kwa wanafunzi.
Katika alfa ya uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam , shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani, ilipata fursa ya kipekee kwa kufungua rasmi huduma hiyo.
Katika uzinduzi huo uliodhuriwa ulioudhuriwa na Naibu Katibu Mkuuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ASelestine Gasimbe aliipongeza Multcoice Tanzania kwa kufanikisha msaada huo ambao utakuwa ni chachu ya maendeleo kwa elimu nchini “Nina hakika kwa msaada huu, wanafunzi watapata kujifunza mambo mbalimbali, na kujenga uwezo mkubwa wa kimaendeleo” alisema Gasimbe.
Naye Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Peter Fauel alisema kuwa kwa kufunga kifaa hicho wanafunzi hao watapata fursa za kujifunza mengi na kufurahia faida mbalimbali kutoka katika chaneli za kifaa hicho. “Kupitia Dstv, hakika mtapata kuona vipindi mbalimbali vya ulimwengu mzima na kuweza kujifunza zaidi kupitia humo” alisema Fauel.
Multichoice Tanzania mbali na shule hiyo ya Sekondari Jangwani, tayari imeweza kufunga na kutoa vifaa mbalimbali katika shule 20 za Tanzania , vifaa hivyo ni pamoja na Satellite ya kisasa, kimang’uzi cha Dstv na televiasheni.
Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa Kampuni hiyo, Barbara Kambogi, alisema kuwa vifaa hivyo ambavyo vimeunganishwa vipindi mbalimbali, vikiwemo vile vya Wanyama, Siasa,Elimu,Taarifa za Habari za makampuni makubwa ya Ulimwengu ikiwemo BBC na vipindi vingine vya maarifa.
Chaneli muhimu watakazo faidika nazo wanafunzi hao na kujifunza mambo mbalimbali ni pamoja na ‘Discovery Cahannel, National Geographic,BBC Word, History Channel na Animal Planet alisema Kambogi.
Mwisho
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa