*Man Utd yatinga kileleni
*Sholes aipeleka Man Utd kileleni
LONDON,
MSHAMBULIAJI nyota wa Mashetani wekundu, Manchester United, Paul Sholes, juzi alipachika goli pekee la ushindi dhidi ya Wolverhampton 0-1 na kuiwezesha kukwea kileleni kwa kufikisha pointi 63.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kuvutia, Man Utd ilicheza bila mfungaji waje tegemeo na kinara wa magoli katika ligi hiyo, Wyne Rooney alikuwa benchi kutokana na kuwa majeruhi ya mguu.
Scholes aliweza kupachika goli hilo pekee katika dakika ya 73 ya mchezo, kufuatia mabeki wa Wolves, kushindwa kuzuia pasi iliyopigwa na Nani, kabla ya kumpatia Scholes katika eneo la hatari na kupachika goli hilo lililomuacha bila majibu golikipa wa Wolve, Marcus Hahnemann.
Kwa matokeo hayo, United imeweza kufikisha pointi 63 huku ikiwa imeshacheza mechi 29 , ikiwa kileleni na kufuatiwa kwa ukaribu na Chelsea na Arsenal zote zinapointi 61 ambapo Chelsea ikiwa nyuma kwa mchezo mmoja ikiwa imeshacheza mechi 28, na Arsenal wao tayari wameshacheza mechi 29.
Mwisho
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa