-KANISA ANGLIKANA LATIKISWA NA KASHFA YA NGONO
-NI BAADA YA MCHUNGAJI KUTUMA SMS ZA MAPENZI KWA MKE WA MUUMINI
-ALIPOPIGIWA SIMU NA KUJULISHWA ALIKATA NA KUTOPOKEA
-WAUMINI WAGAWANYIKA WADAI MAMBO HAYO YANALIDHALILISHA KANISA.
Na Moses Ng’wat,
Dodoma .
KANISA Anglikana Parishi ya Pandambili jimbo kuu la Mpwapwa/Kongwa mkoani Dodoma limetikiswa na kashifa ya ngono baada ya mchungaji kukamatwa ugoni na mke wa muumini wake.
Kufuatia kashfa hiyo uongozi wa juu wa kanisa hilo jimbo kuu la Mpwapwa/Kongwa limeamua kumsimamisha kazi ya uhudumu ya Kiroho katika kanisa hilo kwa kipindi cha miezi mitatu hadi julai, huku kanisa likiendelea na uchunguzi wa kina.
Taarifa za uhakika kutoka wilayani Kongwa zinadai kuwa kashfa hiyo ya mchungaji kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa muumini umezua hofu kubwa na kuwagawa waumini .
Inadaiwa kuwa mchungaji aliyekumbwa na kashfa hiyo ni Petro Namga wa Parishi ya Pandambili jimbo kuu la Mpwapwa /Kongwa baada ya simu ya mwanamke huyo kukutwa na ujumbe mfupi wa mapenzi(sms 6).
Habari zaidi zinaeleza kwamba tukio hilo lilitokea mwanzoni mwa mwezi januari, baada ya mwanamke jina tunalo kukutwa na ujumbe mfupi wa mapenzi katika simuyake ya mkonono ambao ulitoka kwa mchungaji huyo.
Akizungumza na Tanzania Daima mmoja wa waumini wa kanisa hilo , Parishi ya Pandambili ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema kuwa baada ya mwanamke huyo kubanwa alimtaja mchungaji kuwa ndiye humtumia ujumbe huo wa mapenzi.
Alisema kuwa, mume wa mke wa muumini huyo Robert Chitulu, alikuta ujumbe wa kimapenzi katika simu ya mkewe na alipombana zaidi alidai kuwa ujumbe huo ulitkuwa umetumwa na mchungaji huyo ambaye amlikuwa akimtaka kimapenzi kwa muda mrefu.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo Chitulu aliamua kuwaagiza baadhi ya watu kwenda kumueleza mchungaji huyo juu ya tabia yake lakini hakuna kilicho badilika kwani mchungaji huyo aliendelea kumfuatilia mkewe.
Aliongeza kuwa kufuatia mchungaji kuendelea na tabia yake aliamua kumwekea mtego na ndipo alipo mkamata akiwa na mkewe na kuifikisha kesi hiyo katika uongozi wa juu wa kanisa hilo .
“Sasa baada ya huyo mchungaji kubanwa na wazee wa kanisa, kwa mara ya kwanza alikana, lakini walipombana zaidi alikubari na kuomba suluhu ili kuyamaliza kimya kimya.” Alisema Muumini huyo.
Aliongeza kuwa baada ya mchungaji huyo aliyekuwa akihudumia zaidi ya Parishi zisizopungua 10, alishtakiwa kwa msimamizi wa wachungaji (Area Dean) wa jimbo hilo Kasisi Philimon Matandu kwa hatua zaidi.
Alisema baada ya vikao kadhaa vya usuluhishi kati ya mume wa mwanamke aliyefumaniwa, mchungaji na uongozi wa kanisa,vilivyoanzia mwezi januari hatimaye walifikia muafaka, ambapo Februari 25 mwaka huu mchungaji huyo aliamuriwa kulipa faini ya shilingi 100,000.
Aidha, viongozi wa juu ngazi ya jimbo akiwemo Askofu Mkuu walikubaliana kwa pamoja kutoa adhabu ya kumsimamisha mchungaji huyo kuendelea na kazi ya kutoa huduma mpaka uchunguzi wa kina utakapofanyika.
Mchungaji huyo alipopigiwa simu na Tanzania Daima na kujulishwa juu ya suala hilo ghafla alikata simu na alipopigiwa tena simu ilikuwa ikisikika ikiita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Jimbo kuu la Mpwapwa/Kongwa, Dk.Jacob Chimeledya alikiri kutokea kwa hali hiyo na kudai kuwa kanisa limechukua hatua za awali za kumsimamisha kutoa huduma kwa miezi mitatu.
Alisema Uamuzi huo umetokana na uchunguzi wa awali uliofanywa na viongozi wa kanisa hilo ngazi ya jimbo na kwamba baada ya hapo ikibaini hatua zaidi zitachukuliwa kwa kuwa kitendo kilichotokea ni utovu wa nidhamu na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya huduma za kiroho.
Askofu, Dk, Chimeledya alisema kitendo cha mchungaji huyo kimeliaibisha kanisa na kwamba hawezi kuendelea na kazi ya kumtumikia Mungu.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa