Mlinzi anayekiri kumzimia Cafu
Yes! Katika safu ya ‘Chipukizi wa Wiki’ leo tunaye mlinzi wa pembeni (full-back) wa Manchester United, Mbrazil, Rafael Pereira da Silva. Kura nyingi zimemteua yeye awe chipukizi wetu katika safu hii ya Michezo na Wachezaji.
Kipaji kilichomo kichwani na miguuni mwa kijana huyu mwwenye umri wa miaka 20, kimezua gumzo kubwa katika safu ya ulinzi ya Manchester United ambako nahodha wa timu hiyo Garry Neville anaonekana kuelemewa na kasi ya Mbrazil huyu.
Rafael alizaliwa Julai 9, 1990 sambamba na pacha wake Fabio ambaye pia uichezea Manchester United. Walizaliwa katika kitongoji cha Petrópolis jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil.
Beki huyu alikuwa hapo kabla akimudu vema nafasi ya winga kabla ya kubalishwa uelekeo na kurudi nyuma kucheza beki mbili. Urefu wake wa futi 5 na inchi 8 ulichangia kumbadilisha, kwani ulimpa taabu kukabiliana na walinzi warefu.
Mechi ya kwanza kuichezea Man United katika Ligi Kuu ilikuwa ni ya ushindi wa 4-0 dhidi ya West Bromwich Albion Oktoba 18, 2008. Moja ya rekodi zake ni bao la kuvutia liloifunga Arsenal iliyokuwa nyumbani Emirates na kushinda 2-1.
Katika mechi hiyo iliyochezwa Novemba 8, 2008 akifunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu kunako dakika ya 90. Tokea hapo amejijengea jina na heshima miongoni mwa wadau wa klabu hiyo.
Mechi anayoikumbuka; Rafael kamwe hawezi kuisahau mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Everton iliyopigwa Aprili 9, 2009 kwenye uwanja wa Wembley.
Kisichomsahaulisha mechi hiyo si kupoteza kwa penalti 4-2 dhidi ya Everton, bali ni kutimia kwa ndoto yao (yeye na pacha wake Fabio) ya kucheza kwenye kikosi kimoja wote wakianzia kikosi cha kwanza.
Rafael anakiri wazi kuvutiwa na aina ya uchezaji ya beki wa zamani wa kulia wa Brazil, Cafu. Moja ya matarajio yake, ni kuiwezesha Brazil kuendelea kuikamata dunia kwa soka safi na kutwaa vikombe.
Moja ya mafanikio yake ni kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka 2009 iliyokwenda kwa Ashley Young wa Aston Villa.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa