DAKTARI wa Kituo cha Afya Mburahati Barafu, Nicholas Matomola (32), amefikishwa katika Mahakama ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Akimsomea mashitaka hayo, Baseba Kasanga, alidai mbele ya Hakimu Sundi Fima, kuwa Februari 19 mwaka huu, majira ya saa 6 mchana katika Maabara ya B.T. Diagnostic Centre, maeneo ya Mabibo Hostel, alimuua Jubilate Shao (22), alipokuwa akimtoa mimba ya miezi saba.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi za mauaji. Kesi imeahirishwa hadi Machi 11, mwaka huu itakapotajwa tena.
Daktari huyo alifikishwa mahakamani hapo majira ya asubuhi akiwa pamoja na mahabusu wengine kadhaa, huku akionekana kujiamini.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa