RAIS Jakaya Kikwete ametoa zawadi ya vyakula kwa vituo 10 vya kulea watoto yatima na wazee nchini kwa ajili ya Sikukuu ya Maulid.
Akikabidhi zawadi kwa niaba ya rais, Naibu Katibu wake, Shaaban Gurumo, alisema lengo la rais kutoa zawadi hizo ni kuhakikisha jamii yote inasherehekea Maulid kwa upendo na amani.
“Ni kawaida kwa rais kuwazawadia wazee wasiojiweza na yatima katika vituo mbalimbali ili wasijione wanyonge…wanatakiwa kujua kwamba rais anawapenda na kuwakumbuka muda wote,” alisema Gurumo ambaye pia ni Kaimu Mnikulu.
Vituo vyote 10 vilipata mbuzi wawili, lita 20 za mafuta na mchele kilo 100 kila kimoja, zawadi ambazo zilipokewa na wawakilishi wao kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam jana.
Gurumo alivitaja vituo vilivyopewa zawadi hizo ni Tuamoyo Hostel Kigamboni, Chuo cha Ufundi kwa walemavu Yombo, Kituo cha kulea yatima New Life Magomeni, Kituo cha cha yatima VOSA Kongowe na kituo cha yatima Mburahati.
Vituo vingine ni kituo cha wasiojiweza Nunge, Kigamboni, kituo cha yatima Moyo Mmoja Bagamoyo na Kituo cha yatima Ummimuuminim, Vingunguti kwa Tanzania Bara.
Aidha, vituo vingine vilivyopewa zawadi ni kituo cha yatima Forodhani kilichopo Unguja na kituo cha yatima Mabaoni Pemba.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa