Dar es Salaam/Iringa. Siku mbili baada ya Tume
ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kutoa waraka wa
kulitaka Bunge Maalumu la Katiba kutopuuza mapendekezo ya muundo wa
serikali tatu, Askofu Mkuu wa Jimbo Mkuu la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo ameibuka na kusema msimamo huo siyo wa Kanisa
Katoliki nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana, Kardinali Pengo pamoja na kukiri kuwa tume ilitoa maoni hayo,
alikanusha kuwa taarifa zilizotolewa na moja ya magazeti kuwa msimamo wa
Kanisa Katoliki ni serikali tatu.
“Maoni ya Tume hayawezi kuwa ni msimamo wa kanisa.
Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa misimamo yake na huwa inatolewa
na Mwenyekiti wa TEC,” alisema.
Hata hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcisius
Ngalalekumtwa kutoka Jimbo la Iringa, alisema jana kuwa alikuwa na
shughuli nyingi, hivyo asingeweza kuzungumzia suala hilo, labda wiki
ijayo.
kwa taarifa zaidi bofya hapa
kwa taarifa zaidi bofya hapa
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa