Dk. Omary Ubuguyu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) wakati akitoa semina kwa waandishi wea habari kuhusu ugonjwa huo |
Kwa upande wake Mratibu wa semina hiyo ,kutoka Mradi wa Taifa wa Kisukari, John Gardner alisema gharama ya matibabu ya ugonjwa huo ugharimu dola za Marekani milioni 378 ya asilimia 12 ya bajeti ya afya duniani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2010, ambapo inaweza kufikia hadi zaidi dola milioni 400.
Akizungumzia kuhusu ugonjwa huo, Dk. Zakharia Ngoma alisema ulaji usiofaa na mtindo wa maisha huchangia kwa kiasi kikubwa . Hivyo hutumiaji wa vya kula vya asili ,vya kuchemsha, mafuta, chumvi na sukari kidogo , mboga za majani kwa wingi na matunda kila siku , pamoja na vyakula vyenye virutubisho vyote husaidia kuepukana na ugonjwa huu, ” alisema Dk. Ngoma. Aliongeza kuwa hutumiaji wa vyakula vya jamii ya kunde na visivyokobolewa husaidia kuepuka ugonjwa huu, ikiwemo kunywa maji kwa wingi na kuepuka msongo wa mawazo.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa