Translate in your language

Wednesday, February 12, 2014

KISA MVI WAZEE WAULIWA KENYA ....

Je wafahamu kuwa na mvi katika baadhi ya sehemu katika pwani ya Kenya ni hatari kwa usalama na maisha yako?
Hilo limejitokeza huko Kilifi ambako wazee wamekuwa wakiuwawa na watu wasiojulikana kwa kisingizio kuwa ni wachawi.
Kutokana na hilo wazee wasiopungua thelathini wamekimbilia katika kaya iitwayo Godoma ili kuokoa maisha yao.
Kuna wazee wengine wanaodaiwa kuuawa kwa sababu za urithi na familia zao

kwa maoni yangu tofauti na habari, wazee wanauwawa sio kwa sababu ya uchawi, uchawi ni kiini macho tu. vijana wanaua wazee wao kisa warithi mali na kutajilika bila kufanya kazi, uchunguzi zaidi ufanyike, na pia kuua ni jinai wasifikiri kigezo cha uchawi kitaondoa hiyo jinai na kwa wale walio na imani kama mimi mwisho wa dunia kuna kuulizwa kutokana na madhalimu ya kidunia tuliyofanya 

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)