Translate in your language

Saturday, December 7, 2013

Viongozi wa kiafrika wamlilia Madiba

Viongozi mbali mbali barani Afrika nao wametoa rambi rambi zao na kumwelezea Nelson Mandela kama mfano mwema kwao, wakisema pengo lake haliwezi kuzibwa kirahisi.



Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika Dr Dramini Nkosazana Zuma amesema kifo cha Nelson Mandela ni pigo si kwa Afrika Kusini na Afrika tu, bali kwa jamii nzima ya binadamu.
Bi Zuma amesema kuwa Mandela alikuwa alama ya mshikamano katika mapambano ya umma dhidi ya utawala dhalimu wa ubaguzi wa rangi, unyanyasaji na ukoloni, na kuitolea wito Afrika wa kukumbatia yale aliyoyathamini.
Rais wa Halmashauri kuu ya AU, Nkosazana Dlamini Zuma
Rais wa Halmashauri kuu ya AU, Nkosazana Dlamini Zuma
Nchini Tanzania siku tatu za maombolezo zimetangazwa kuomboleza kifo cha Nelson Mandela. Rais wa Tanzania Nelson Mandela amemtaja marehemu Mandela kuwa sauti ya ushujaa na chanzo cha hamasa, na kuongeza kuwa ni kipenzi cha watu aliyetoa mfano mwema.
Katika nchi jirani ya Kenya, rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyata amesema Mandela alikuwa kiongozi alitoa matumaini na mwenye kutoa msukumo wa maridhiano. Kenyatta amesema maisha ya Mandela yanatoa somo muhimu kuwa nguvu ya dhamira inaweza kuugeuza uhasama kuwa ushindi.

kwa taarifa zaidi bofya hapa 

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)