Translate in your language

Tuesday, November 12, 2013

Dr. Sengondo Mvungi amefariki dunia hospitalini South Africa.

Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.
Ni jana tu ambapo Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi alitangaza kushikiliwa kwa watu tisa wanaotuhumiwa kuhusika na ujambazi uliofanywa dhidi ya Dr. Sengondo Mvungi aliekua mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na kiongozi wa NCCR-Mageuzi.
Tayari viongozi mbalimbali kama Mh. Warioba, Katibu wa tume, naibu na watumishi wengine wachache wammueekwenda nyumbani kwa marehemu

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)