Translate in your language

Tuesday, August 6, 2013

Uchaguzi Zimbabwe wazua maoni tofauti

Baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa, Zimbabwe inaelekea katika wakati mgumu wa kisiasa. Waangalizi wa SADC na Umoja wa Afrika wasema uchaguzi umekwenda vizuri; nchi za Magharibi zakosoa hitilafu.
"Robert Mugabe achaguliwa tena kuwa rais!" Kichwa hicho cha habari kilitawala magazeti mengi ya Kiafrika hapo jana baada ya tume ya uchaguzi ya Zimbabwe kutangaza kuwa Mugabe amepata asilimia 61 ya kura na hivyo kumwacha mbali kabisa mpinzani wake wa karibu Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC. Yeye aliambulia asilimia 34 tu ya kura.
Miongoni mwa viongozi wa kwanza kumpongeza Mugabe, mwenye umri wa miaka 89, alikuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Alitoa pongezi zake za dhati na kuzitaka pande zote kukubali matokeo ya uchaguzi kama matakwa ya wananchi wa Zimbabwe.
Lakini kutoka nchi za Magharibi, Mugabe hakupokea pongezi. Wengi wanashuku uhalisia wa matokeo kutokana na shutuma za wizi wa kura zilizozushwa na wafuasi wa chama cha MDC na vile vile mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyokuwa yakifuatilia maandalizi ya uchaguzi kwa karibu.
kwa taarifa zaidi bofya hapa

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)