VINARA Yanga, leo watafikisha pointi 42 kileleni mwa msimamo na kuwaacha mbali mahasimu wao na mabingwa watetezi Simba, iwapo wataifunga Kagera Sugar katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kabla hata ya mchezo huo wa leo, Yanga tayari wameandika pengo la pointi nane dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 31.
Mahasimu wao, Simba ni wazi wamechomoka kwenye mstari wa mbio za ubingwa baada ya juzi kupata kipigo wasichokitarajia cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar.
Kipigo hicho cha kwanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na cha tatu msimu huu, kimeifanya Simba kuendelea kutoa mwanya kwa Yanga na Azam kufukuzana kileleni.
chanzo: mwananchi gonga hapa kwa taarifa zaidi
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa