MWANDISHI WETU
SIMBA inahitaji kushinda mechi zake zote nane zilizosalia kwenye mzunguko wa pili kufikisha pointi 55 lakini ikiombea angalau Yanga ikipoteze mechi tatu mfululizo na Azam ikipoteze mbili na kutoa sare.
Azam yenye pointi 36 ikishinda mechi zake zote zilizosalia itakomea kwenye pointi 60 wakati Yanga ikifanya hivyo hivyo itamaliza na pointi 66 ambazo Simba haiwezi kuzifikia kwa sasa.
Uchunguzi uliofanywa na Mwanaspoti kuhusiana na mwenendo wa Simba umebaini mambo makubwa sita ambayo ni kikwazo kwa Simba ndani na nje ya uwanja na kupelekea timu hiyo kuyumba kiasi cha kuhatarisha utetezi wa ubingwa wake.
Benchi la ufundi
Uchunguzi unaonyesha kwamba kumeibuka mgawanyiko baina ya wachezaji ambapo baadhi hususani wakongwe wanadai hawamuelewi Kocha Mkuu, Patrick Liewig na walipendelea kuendelea kufanya kazi na Mserbia aliyetimuliwa Milovan Cirkovic.
chanzo: mwanaspoti gonga hapa kwa taarifa zaidi
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa