Translate in your language

Thursday, February 7, 2013

STARS NA CAMEROON KATIKA PICHA - TAIFA, ILIKUWA FULL SHANGWE

 Wa Mazembe, si wazembe; Thomas Ulimwengu akimpongeza mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta kuifungia Stars leo
 Mbwana Samatta wa Tanzania akifunga bao baada ya kumlamba chenga kipa wa Cameroon, Efalla Komguep katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa baina ya timu hizo jioni ya leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tanzania, Taifa Stars ilishinda 1-0.
 Beki wa Stars, Erasto Nyoni akimtoka beki wa Cameroon, Assou Ekotto
 Thomas Ulimwengu akiwa ameruka juu na kipa wa Cameroon, Efalla Komguep kuwania mpira wa juu
 Kiungo Frank Domayo wa Tanzania kulia akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Cameroon, Nyom Allan
 Mbnwana Samatta akipambana na mabeki na kipa wa Cameroon
 Thomas Ulimwengu akiwalamba chenga mabeki wa Cameroon
 Kikosi cha Stars

 Wachezaji wa Tanzania wakishangilia bao lao lililofungwa na Samatta waliyemdandia
 Beki Pierre Wome wa Cameroon akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Samatta, huku  Ekotto kulia akiwa tayari kutoa msaada
 Beki Shomary Kapombe akitia krosi huku beki wa Cameroon, Nyom Allan akiipisha
 Beki wa Cameroon, Assou Ekotoo akimiliki mpira mbele ya kiungo Mrisho Ngassa wa Tanzania
Hapa ndipo Stars ilipopata penalti, beki Ngoula aliupitia mpira miguuni mwa Samatta akitokea nyuma ndani ya eneo la hatari

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)