Watu nane wenye silaha wameteka basi la Sumry baada ya kuweka kizuizi
cha magogo na mawe katika msitu wa Msaginya ulioko katika Mkoa wa
Katavi, maeneo ya barabara kuu ya Sumbawanga – Mpanda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, amesema
uhalifu huo ulifanyika saa sita usiku wa kuamkia jana wakati basi hilo,
usajili T107 BHT, likisafiri kutoka Sumbawanga kuelekea Mpanda.
Alifafanua kwamba dereva alilazimika kusimamisha basi baada ya
kukumbana na vizuizi hivyo, basi lilipofika eneo hilo lenye mteremko na
kona kali. Inadaiwa kwamba watu nane waliibuka kutoka mafichoni wakiwa
na silaha za jadi zikiwamo mapanga, nondo, mawe na visu na kuwalazimisha
abiria wote kushuka. Waliwapekua na kuwapora abiria hao simu za mkononi
15 na kiwango kikubwa cha fedha.

kwa taarifa zaidi bofya hapa
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa