miwa
na U.S.A kuwa alikua anaunga mkono harakati za Al Shabaab, tukio ambalo
lilisababisha maandamano na ghasia mjini Mombasa. Wateteaji wa haki za
binaadamu wamesema mauaji ya Sheikh Rogo ni mfano wa mauaji yasiyokuwa
ya halali, ya kuchukua hatua mkononi na kuua watuhumiwa wa ugaidi kabla
hawajapatikana na hatia mahakamani; matukio ambayo yanasadikiwa
kuendeshwa na polisi wa kenya.
Mji wa Mombasa nchini Kenya umekumbwa na vurugu kufuatia kuuawa
kwa mhubiri wa dini ya Kiislamu Aboud Rogo Mohammed, ambaye alihusishwa
na makundi ya Kigaidi.
Mamia ya vijana wenye hasira walifanya vurugu katika mji wa Mombasa,
wakirusha mawe na kuharibu magari huku wakielekea katikati ya mji huo.
Machafuko hayo ni mwendelezo wa yale yaliyozuka Jumatatu, mara baada ya
kuuwawa kwa mhubiri Aboud Rogo, ambaye kwa mujibu wa polisi
alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Rogo alikuwa katika
orodha ya watu waliowekewa vizuizi na Marekani na Umoja wa Mataifa kwa
tuhuma za kuliunga mkono kundi la al-Shabaab lenye mafungamano na kundi
la kigaidi la al-Qaeda
kwa taarifa zaidi bonyeza hapa
2 comments :
Allah aiweke roho ya Sheikh wetu PEPONI Amin! madhali alikuwa mtoa daawa mzuri kila jema litakuwa juu yake inshallah.
Mungu amrehemu huko aliko amin
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa