SENSA ya Watu na Makazi jana iliingia siku yake ya pili, huku kasoro
kadhaa ikiwamo ukosefu wa vifaa, upungufu wa makarani na watu kugoma
kuhesabiwa vikiripotiwa.Katika baadhi ya maeneo hadi jana, wananchi
walikuwa hawajaanza kuhesabiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana
na ukosefu wa vifaa na makarani.
Ofisa Uhamasishaji wa Sensa
Taifa, Said Ameir alikiri kupata taarifa za kasoro hizo lakini akaeleza
kushangazwa na chanzo chake, akisema: “Vifaa tulivigawa maeneo
mbalimbali nchini kulingana na mahitaji. Tunashangazwa na taarifa hizo
kwamba hata wengine wamekosa reflector (makoti ya kuakisi mwanga) na
vitambulisho.”
“Tunachofanya sasa ni kuchunguza tatizo hilo
limeanzia wapi na limesababishwa na nini. Vilevile tunajitahidi
kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinapelekwa sehemu hizo ili kazi hiyo
iendelee kama kawaida.”
taarifa zaidi bonyeza hapa
2 comments :
I used to be recommended this web site through my cousin.
I'm not positive whether this put up is written via him as nobody else recognize such designated approximately my trouble. You're amazing!
Thanks!
Also visit my website - Fat Loss Factor Reviews
You need to be a part of a contest for one of the highest quality websites on the internet.
I am going to recommend this blog!
My blog post : cardio exercises
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa