Mtuhumiwa wa mauwaji ya watu 77 nchini Norway Anders Behrings Breivik amehukumiwa kifungo cha miaka 21 jela. |
Breivik aliwauwa kwa bomu watu wanane mjini Oslo na baadae kuwauwa vijana wengine 69 kwa kuwafyatulia risasi vijana wa chama cha Labour kwenye kambi waliyokuweko karibu na kisiwa cha Utoya Julai 22 mwaka jana.
Kisheria Norway haina adhabu ya kifo wala kifungo cha maisha na kiwango cha juu kabisa cha adhabu kwa Breivik ni miaka 21. Hata hivyo wafungwa kama Breivik kama wakionekana kuwa wataendelea kuwa kitisho kwa jamii muda wa kukaa gerezani unaweza kuongezeka.
kwa taarifa zaidi bonyeza hapa
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa