MKAZI wa Tuliani, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro (jina linahifadhiwa), amelazimika kujifungulia katika chumba cha mlinzi wa Hospitali ya Rufaa mkoani hapa, baada ya kucheleweshwa na walinzi wa hospitali hiyo ambao walikuwa wakimuhoji.
Mama huyo alikwenda hospitalini hapo kumtembelea ndugu yake lakini alipatwa na uchungu wa ghafla akiwa njiani hivyo alimua kwenda Kituo cha Afya Nunge lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya, walimchukua na kumpeleka Hospitali ya Mkoa huo.
Kwa mujibu wa Bw. Coroneli Mwilongo, ambaye ni ndugu wa mama huyo, alisema baada ya kufika kwenye mlango wa hospitali hiyo waliomba kuingia ndani lakini mazungumzo kati yao na walinzi yalikuwa marefu hadi alipozidiwa.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Bi. Ritha Lyamuya, amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai kuwa, mama huyo alikwenda Kituo cha Nunge ambako baada ya kupimwa, alikutwa mapigo yake ya moyo yako juu.
“Mimi nilipata habari hii saa nne asubuhi, nilipokwenda eneo la tukio nilikuta tayari ameshajifungua, mama huyu pamoja na mtoto wake wanaendelea vizuri,” alisema.
Aliwataka wanawake wajawazito kuwahi mapema hospitalini mara wanaposhikwa na uchunguna pamoja na kutembea na vifaa vya kujifungulia miezi yao ya kujifungua inapokaribia.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa