Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakimsubiri Rais Kikwete kuja kutangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete akitangaza majina ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo. Wakishuhudia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi na Waziri wa Sheria na Katiba Mama Celina Kombani.
Rais Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakitoka chumba cha mikutano Ikulu baada ya Rais kutangaza wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Rais Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoitangaza, akisisitiza kwamba tarehe ya kuanza kazi itatangazwa rasmi mara baada ya wajumbe wote kujulishwa uteuzi wao na baadae kuapishwa. Ila kisheria tume inatakiwa iwe imekamilisha kazi ndani ya miezi 18.
PICHA ZOTE NA IKULU
TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
(Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,
Toleo la 2012, Vifungu 5, 6 na 7)
______________________________
UONGOZI WA JUU
1. Mhe. Jaji Joseph Sinde WARIOBA - Mwenyekiti
2. Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino
RAMADHANI - Makamu Mwenyekiti
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - BARA
1. Prof. Mwesiga L. BAREGU
2. Nd. Riziki Shahari MNGWALI
3. Dr. Edmund Adrian Sengodo MVUNGI
4. Nd. Richard Shadrack LYIMO
5. Nd. John J. NKOLO
6. Alhaj Said EL- MAAMRY
7. Nd. Jesca Sydney MKUCHU
8. Prof. Palamagamba J. KABUDI
9. Nd. Humphrey POLEPOLE
10. Nd. Yahya MSULWA
11. Nd. Esther P. MKWIZU
12. Nd. Maria Malingumu KASHONDA
13. Mhe. Al-Shaymaa J. KWEGYIR (Mb)
14. Nd. Mwantumu Jasmine MALALE
15. Nd. Joseph BUTIKU
WAJUMBE KUTOKA TANZANIA - ZANZIBAR
1. Dkt. Salim Ahmed SALIM
2. Nd. Fatma Said ALI
3. Nd. Omar Sheha MUSSA
4. Mhe. Raya Suleiman HAMAD
5. Nd. Awadh Ali SAID
6. Nd. Ussi Khamis HAJI
7. Nd. Salma MAOULIDI
8. Nd. Nassor Khamis MOHAMMED
9. Nd. Simai Mohamed SAID
10. Nd. Muhammed Yussuf MSHAMBA
11. Nd. Kibibi Mwinyi HASSAN
12. Nd. Suleiman Omar ALI
13. Nd. Salama Kombo AHMED
14. Nd. Abubakar Mohammed ALI
15. Nd. Ally Abdullah Ally SALEH
UONGOZI WA SEKRETARIETI
1. Nd. Assaa Ahmad RASHID - Katibu
2. Nd. Casmir Sumba KYUKI - Naibu Katib
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa