DJ Kim kuwasha moto miaka 15 Loyola High School.
Na Mwanablog Wetu Dar
DJ Kim kupagawisha shoo ya kusherekea miaka 15 ya shule Loyola High School maalufu kama "-Loyolites and Friends Re-Union Party" itakayofanyika jioni ya Julai 31 ndani ya ukumbi wa Jangwani sea Breeze.
Akiongea na Mafia Blog leo jijini Dar es Salaam mratibu wa jumuiya ya wanafunzi waliosoma Loyola (Loyola Alumni Assocition) "LAA" Glen Kapya alisema kuwa lengo la sherehe hiyo ni kuunganisha umoja kwa wanafunzi waliosoma shuleni hapo na kudumisha ushirikiano na umoja.
"Kila mwaka tunafanya sherehe hizi ambazo ni maalum kujumuika pamoja na kubadilishana mawazo ndani ya jumuiya yetu' alisema Glen.
Hivyo aliwataka wanafunzi wote waliosoma Loyola kujitokeza kwa wingi hiyo Julai 31 shuleni hapo kisha kujumuika katika tafrija hiyo Jangwan Sea Breeze na kusherehekea kwa pamoja.
Glen alisema tiketi ya 'party' hiyo ni shilingi 30,000 ambayo imejumuisha chakula, usafiri, kiingilio,muziki na vinywaji. "Tunaomba kujitokeza kwa wingi ilikufanikisha 'party' hii na tiketi zinapatikana hapa shuleni Loyola, Maika Elegaant Wear, Benjamin Mkapa Towers ,Mezai nnefloor(posta), Engen Petrol Station (Ubungo).
Aidha katika party, hiyo alisema kuwa DJ Kim atapagawisha muziki mkali na kukonga nyoyo huku kukiwa na kila aina ya burudani pamoja na matukio maalum yaliyoandaliwa na LAA.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa