Translate in your language

Thursday, January 22, 2015

GUSA GUSA MIN BAND NDANI YA OLD IS GOLD SAFARI CARNIVAL KILA JUMAPILI

Gusa Gusa Min band  ndani ya Usiku wa Old is Gold Safari Carnival kila J2

Na Andrew Chale
Bendi ya taarab ya 'Gusa Gusa Min Band,'  inatarajiwa kurindima kila Jumapili katika usiku wa Old is Gold Taarab ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikochezni B, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, kila Jumapili bendi hiyo ya Gusa Gusa itakuwa ikitoa burudani ya kipekee kwa  nyimbo za taarab zikiwemo za zamani na zile za kisasa.
"Kila jumapili  kwa kiingilio cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa mwambao  watafurahia bendi ya Gusa Gusa ndani ya Usiku wa Old is Gold katika ukumbi wa Safari Carnival" alisema Asia Idarous.
Asia Idarous amewasihi wapenzi na wadau kujitokeza kwa wingi kushuhudia bendi hiyo pamoja na kukumbushana yale ya zamani na kubadilishana mawazo.
Mdau huyo Asia Idarous aliongeza kuwa, usiku huo uliodhaminiwa na  Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo, utakuwa wa aina yake kwa kila atakayefika ukumbini.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)