Translate in your language

Saturday, January 3, 2015

Palestina kuwasilisha ombi la kujiunga ICC

Palestina inatazamiwa kuwasilisha rasmi maombi ya kujiunga na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kufuatia hatua ya Rais Mahmoud Abbas kusaini mkataba wa mahakama hiyo mjini The Hague.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliitolea wito ICC kulikataa ombi la Palestina kujiunga na mahakama hiyo, aliloliita la kinafiki. Kwa mujibu wa Netanyahu, serikali ya Mamlaka ya Palestina si dola, bali kundi lililounda ushirikiano na kundi jengine la kigaidi, Hamas, ambalo linafanya uhalifu wa kivita.
"Israel ni dola linalofuata sheria na lenye jeshi lenye maadili linaloheshimu sheria zote za kimataifa. Tutawalinda wanajeshi wetu kama wao wanavyotulinda sisi." Ilisema taarifa iliyotolewa na ofisi ya Netanyahu, baada ya kikao cha dharura kwenye makao makuu ya wizara ya ulinzi hapo Alhamisi.
Siku ya umatano, Rais Abbas alisaini mkataba wa ICC na makubaliano mengine 19 ya kimataifa, kufuatia hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku moja nyuma, kulikataa pendekezo la Palestina kuitaka Israel ikomeshe ukaliaji wake kufikia mwaka 2017.

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)