Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 6 wako katika hali mbaya kati ya majeruhi 17 wa ajali ya moto uliosabiashwa na watu waliokuwa wakiiba mafuta baada lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta ya Petroli kuanguka karibu na makazi ya watu eneo Mbagala Charambe jijini Dar es salaam.
EATV imefika katika eneo hilo na kushuhudia mabaki ya lori lililokuwa limebeba mafuta ya Petroli huku maduka yaliyokuwa yamezunguka nyumba ya kulala wageni yakiwa yameteketea kwa moto wa Petroli uliosababishwa na baadhi ya watu waliokuwa wakiiba mafuta bada ya lori lililobeba mafuta kuanguka usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa miongoni mwa waathirika hao alichomoa Betri ya lori hilo na kusababisha mlipuko wa mafuta.
Kutokana na moto huo baadhi ya wafanyabiashara waliopoteza mali zao ambapo wengine mpaka sasa hawajajua thamani ya mali zililotekea ambapo mmoja wa wafayabiashara Bwana Ali Mohamed mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi amedai kupoteza malizenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 70, huku wengine wakitaka bima ya lori itumike kufidia mali zilizopotea.
Akielezea tukio lilivyotokea mmoja wa wagonjwa Bwana Rajabu Selemani amesema baadhi ya watu walioungua akiwemo yeye alikuwa anapita barabarani akitokea kazini ndipo alipokuta barabara imetapakaa mafuta ya petroli na baadaye moto mkali ghafla ukaanza kuwaka na kuwaunguza miguuni.
Muuguzi wa zamu wa hospitali ya Temeke, Bi Rolesta Kinonda amesema hospitali wamepokea maiti 1 ya mwanaume, majeruhi 20, 19 wanaume na mwanamke ambapo kati ya majeruhi hao wanne wamewabakiza hospitalini hapo na mwanamke ameruhusiwa baada ya kupata huduma ya kwanza.
Akizungumizia tukio hilo baada ya kutembelea wagonjwa katika hosptali ya taifa ya Muhimbili na hospitali ya Temeke, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bwana Said Mecky Sadicki amewataka wananchi wasikimbile kuiba mafuta wakati malori ya mafuta yanapoanguka.
chanzo_ East Africa News
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa