Sehemu
ya kwanza
Mtoa wa chanjo akitoa chanjo kwa mtoto |
Kampeni ya chanjo dhidi ya surua na rubella
UTANGULIZI
Tanzania imekuwa
ikifanya vizuri katika mikakati ya kupunguza vifo vya watoto ili kufikia lengo
la nne (4) la milenia la kupunguza vifo vya watoto. Mojawapo ya mikakati hiyo
ni utoaji wa chanjo kwa watoto ili kuwakinga na magonjwa yanayozuilika kwa
chanjo.
Tanzania ni moja kati
ya nchi ambayo ina utaratibu madhubuti wa kufanya kampeni za kitaifa za utoaji
wa chanjo. Kampeni ya mwaka 2014 ina lengo la kutoa chanjo ya Surua Rubella,
matone ya Vitamini A. Vilevile Kingatiba za Minyoo, Mabusha na Matende kwa
kutumia dawa za Albendazole na Ivermectin zitatolewa.
Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeandaa kampeni ya
kitaifa ya kutoa;
- Chanjo ya
Surua Rubella kwa watoto wote walio katika umri wa miezi 9 mpaka chini ya
miaka 15
- Kutoa
vidonge vya vitamin A kwa watoto wote wenye umri wa miezi 6 mpaka 59
- Kutoa dawa
za minyoo aina ya Mebendazole kwa watoto wote wenye umri wa miezi 12 hadi 59.
- Kutoa dawa
za minyoo aina ya Albendazole kwa umri wa miaka 5 na kuendelea kwa mikoa
husika.
- Kutoa dawa
ya Ivermectin na Albendazole zinazokinga Usubi, Minyoo ya Tumbo, Matende
na Mabusha kwa umri wa miaka 5 na kuendelea kwa mikoa husika.
Kampeni hii
itafanyika kwa utaratibu wa watoto wote wenye umri chini ya miaka kumi na tano
kupelekwa katika vituo vya kutolea huduma vilivyoandaliwa. Pia kampeni hii
itahusisha watoto walio shuleni na wale wasio shuleni na watu wa umri wa zaidi
ya miaka 15 kwa dawa za Albendazole na Ivermectin
SIKU
ZA KAMPENI
Kampeni itafanyika
kitaifa kwa siku saba (7) kuanzia tarehe 18 mpaka 24, Octoba, 2014.
AINA ZA VITUO:
Kampeni
ya hii itafanyika katika vituo vya uchanjaji vya aina mbili
·
Vituo
vya kudumu – Timu za uchanjaji zitakuwa kwenye kituo kwa siku saba (7) kuanzia
saa 1asubuhi hadi saa 11 jioni.
·
Vituo vya muda na kuhama hama - timu za uchanjaji
huduma kwa tarehe zilizopangwa na zikimaliza walengwa katika eneo husika
zinahamia sehemu nyingine iliyopangwa.
LENGO
LA KAMPENI YA KITAIFA
·
Kuna
uthibitisho wa kitaalamu kwamba ni asilimia 85 tu ya watoto wanaopata chanjo ya
surua wakati wanapotimiza miezi 9 wanapata kinga kamilifu ya ugonjwa wa surua.
·
Kuna
watoto wengine ambao hawajapata kabisa huduma ya chanjo na kuna vituo ambavyo
havijafikia lengo la kuwachanja watoto kwa asilimia 100. Mlundikano wa watoto
hawa wasio na kinga kila baada ya miaka 3 hadi 4 huweza kusababisha milipuko ya
ugonjwa wa surua.
·
Tafiti
zilizofanyika nchini zinaonesha kwamba ugonjwa wa Rubella upo na umeathiri
watoto wengi wanaozaliwa na pia unaleta madhara ya kudumu kwa watoto hawa. Kwa
sababu hiyo ni muhimu chanjo itolewe kuzuia ugonjwa huu na madhara yake.
·
Kampeni
ya kitaifa ya chanjo ya Surua Rubella itawafikia watoto wote wale ambao
hawakupata chanjo ya surua kabla na wale ambao hawakupata kinga kamilifu ili
kuzuia milipuko ya ugonjwa wa surua Rubella.
·
Tafiti
mbalimbali zimethibitisha kuwa watoto wengi walio na umri chini ya miaka mitano
wanakosa virutubisho vya vitamin A ambavyo ni muhimu kujenga na kuulinda
mwili. Vile vile mazingira wanayocheza
husabibisha wapate minyoo kwa urahisi na kusababisha kudhoofika katika ukuaji
na kupungukiwa damu.Utoaji wa vitamin A na dawa za minyoo utahakikisha watoto
walio chini ya miaka mitano wanapata vitamin A na dawa za kuua minyoo.
·
Kuna
uthibitisho kuwa kila wilaya nchini ina maambukizi ya magonjwa ambayo
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele. Magonjwa haya ni pamoja na Ukoma,Tauni,Kichaa
cha Mbwa,Matende, Mabusha,Trakoma,Kichocho,Usubi,Homa ya Dengue, Minyoo ya
Tumbo,Homa ya Malale na Homa ya Ini. Magonjwa haya yanasabisha ukuaji duni kwa
watoto, ulemavu, upunguzu wa damu mwilini, upofu,uharibfu wa ngozi,
saratani ya kibofu n.k
·
Inakadiriwa
takribani watu milioni 40 wapo katika hatari ya kuambukizwa na watu million 5
wameathirika na magonjwa haya nchini Tanzania. Magonjwa haya hudhibitiwa kwa
njia mbalimbali ikiwamo ugawaji wa dawa (Kinga-Tiba) kwa jamii nzima.Kampeni
hii imelenga pia kudhibiti Matende,Mabusha,Usubi na Minyoo ya Tumbo kwa kutumia dawa za Albendazole na Ivermectin katika mikoa ya
Dar-es-salaam,
Njombe, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Morogoro, Tanga, Tabora, Katavi, Rukwa, Mtwara,
Lindi, Pwani, Manyara, Singida, Dodoma.
Tuungane sehemu ya pili kujua kwa undani magonjwa
haya surua na rubella ikiwemo kinga, tiba, madhara yake nk.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa