Magonjwa ya kuharisha husababishwa na vimelea vya aina mbalimbali. Virusi vya Rota huchangia kwa kiwango kikubwa katika magonjwa ya kuharisha kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.Kiasi cha asilimia 40 ya watoto huambukizwa wakiwa na umri wa chini ya mwaka mmoja lakini mara nyingi watoto wenye umri kati ya miezi 6 na 11 huathiriwa zaidi na ugonjwa huu.
Kuharisha kunakosababishwa na virusi vya rota kunazuilika kwa chanjo inayoitwa Rotavirus, kudumisha usafi wa mazingira,unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita, na utumiaji wa maji safi na salama.Chanjo ya rotavirus imethibitishwa ubora na usalama wake na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Vimelea vya pneomococcal husababisha magonjwa mengi hatari, kati ya magonjwa hayo ni homa ya kichomi (nimonia), homa ya uti wa mgongo, uambukizo wa bakteria kwenye damu (bacteremia). Magonjwa mengine yanayosababishwa na vimelea hivi ni pamoja na ugonjwa wa masikio, magonjwa ya pua (sinusitis)
Magonjwa haya yanaenea kwa kasi, yanatibika iwapo yatagundulika mapema na yanaweza kuzuilika kwa njia ya chanjo.
Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina utaratibu madhubuti wa kutoa chanjo kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja.Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kuzingatia umuhimu wa kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo imeongeza chanjo ya Rotavirus na Nimonia (PCV13) katika Mpango wa Chanjo wa Taifa. Chanjo hizi zimeingizwa katika utaratibu wa chanjo za kawaida za watoto.
ni vizuri kujua chanzo ilivyo, namna ya kuitunza, jinsi ya kuitumia na tahadhari zinazotakiwa kuchukuliwa wakati wa utoaji wake. Inashauriwa kwamba mtoa chanjo asome miongozo na aelewe vizuri kabla hajaanza kutoa chanjo hizi.
thanks! if we play our role we can .....
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa