Translate in your language

Tuesday, April 16, 2013

Mwisho wa bilionea Sambeke; Ni mfanyabiashara maarufu aliyefariki kwa ajali ya ndege.....!!!!!

Arusha/Moshi. Kwa mara nyingine, Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha imetikiswa, kutokana na kifo cha mfanyabiashara maarufu katika mikoa hiyo, Joseph Sambeke (49) maarufu kama Bob Sambeke.
Bob Sambeke alifariki dunia juzi jioni baada ya kuanguka na ndege ndogo aliyokuwa akiiendesha, kilomita moja kutoka Uwanja wa Ndege wa Arusha wakati akitokea mkoani Kilimanjaro.
Huu ni msiba wa tatu katika muda wa mwezi mmoja kwani mwishoni mwa mwezi jana, Wakili na Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Nyaga Mawalla alifariki dunia, ikiwa ni siku moja tagu kufariki ghafla kwa mfanyabiashara mwingine wa madini wa mkoani humo, Henry Nyiti.
Ndege ya Sambeke aina ya MT 7- namba 5H-QTT ilianguka saa 12.34 jioni baada ya bawa lake kugonga mti katika eneo la Magereza linalopakana na uwanja huo.
kwa taarifa zaidi bofya hapa 

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)