MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya
sh.bilioni 5 kwa madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya
kujenga jengo la maegesho ya magari.
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo
Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa
alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la
ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya
magari katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima
katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar es Salaam limekuwa
likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa jengo hilo la kwanza
kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji
letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya
ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema
Silaa.
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio
maana imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka
kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa
msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa
manufaa kwa Watanzania wote
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa