| Patricia Kimelemeta (Gazeti Mwananchi) JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewafikisha kwenye Kamandi ya Wanamaji Dar es Salaam (Navy) maharamia saba, waliotaka kuteka meli ya Sam S Allgood inayofanya utafiti wa mafuta Kaskazini Mashariki mwa Kisiwa cha Mafia.Maharamia hao walikamatwa Oktoba 3, mwaka huu saa 2:00 usiku umbali wa kilomita 40 mwa Kisiwa cha Mafia, Mkoa wa Pwani, wakiwa na silaha wakitaka kuteka meli hiyo. Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Kapambala Mgawe, alisema kutokana na hali hiyo, maharamia hao watahojiwa ili kubaini chanzo cha utekaji huo, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. Kanali Mgawe alisema hadi sasa hawajafahamu nchi wanayotoka maharamia hao, licha ya kuonekana kuwa na asili ya Kisomalia, jambo ambalo limewafanya wawe karibu nao ili waweze kuwahoji kwa undani zaidi. |
Translate in your language
Showing posts with label Maharamia saba waliokamatwa Mafia wapelekwa Navy K’mboni. Show all posts
Showing posts with label Maharamia saba waliokamatwa Mafia wapelekwa Navy K’mboni. Show all posts