Translate in your language

Saturday, July 3, 2010

ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL 2010

Wakazi Zanzibar kushuhudia tamasha la ZIFF bure!!
**Nchi 43 kushiriki tamasha hilo mwaka huuMkurugenzi wa Tamasha hilo, Martin Mhando akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maatayarisho ya ZIFF 2010

 Tamasha kubwa la Utamaduni katika Ukanda wa Afrika Mashariki (Zanzibar International Film Festival ZIFF) linatarajia kuzindulia Julai 10 na kumalizika Julai 18 mwaka huu mjini Zanzibar likishirikisha takribani nchi 43.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, katika ukumbi wa utamaduni wa Alliance Francaise, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Martin Mhando, alisema, Tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka ni nafasi pekee kwa Wazanzibar kujumuika pamoja kutazama filamu zenye viwango ambapo mwaka huu zitaonyeshwa bure.

Kufuatia mwaka huu Zanzibar inatarajia kufanya uchaguzi Mkuu na miaka ya nyuma imewahi kukumbwa na ghasia kauli mbiu itakua ni kuhimiza amani na utulivu kwa Wazanzibar.

Mhando alisema Filamu ya ufunguzi mwaka huu itakua I bring What I Love ya mwanamuziki mkongwe Barani Afrika, Youssou N’dou kutoka nchini Senegal.

Kwa upande wake Mratibu wa Masuara ya Muziki wa ZIFF, Edward Lusala, aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kushuhudia tamasha hilo ambalo litakuwa la kipekee mwaka huu.

Lusala aliwataja baadhi ya wasanii watakao panda katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na; Dully Sykes, AY, Kidumu kutoka nchini Burundi na bendi ya Body Mind Soul kutoka kaskazini mwa Malawi.

Kwa upande wa wasanii waalikwa katika filamu wakiwa ni Steven Kanumba na Ivorry Chery Monalisa. ambao wanatesa na filamu mbali mbali nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.



Filamu ya I bring What I Love, imedhaminiwa na SIGNIS.


..

Press ; Taarifa zaidi-ZIFF

 
Tamasha hili ni kubwa kuliko yote ya utamaduni ya aina yake kwenye ukanda wa Afrika mashariki. Ikiwa imetimiza miaka 13 na kuudhuriwa kila mwaka na zaidi ya wageni 200,000 na kushirikisha nchi 43,
ZIFF ni taasisi ya wazanzibari yenye kulenga zaidi filamu za kiafrika huku ikisherehekea na kuthamini utajiri wa tamaduni zilizopo ndani ya ukanda huu na zaidi
 Tofauti na tamasha lingine lolote, hili ni tajiriba ya aina yake ya tamaduni za kiafrika. Hakuna zuria jekundu, Umaridadi na waandishi wa habari za udaku.

ZIFF ni tamasha linalokuja mara moja tu kwa mwaka, ni nafasi ya pekee kwa Wazanzibari kujumuika pamoja na kutazama filamu kwenye viwambo vikubwa. Kwa mwaka huu filamu zote zitaonyeshwa bure kwa wakazi wote wa Zanzibar!


ZIFF’s theme this year’s is Hopes in Harmony.


Mwishoni mwa mwaka huu Zanzibar itafanya uchaguzi mkuu wa serikali.
una historia ya machafuko kipindi cha uchaguzi kwa kutazama uchaguzi uliopita mwaka 2005 kati ya wanaounga mkono upinzania na polisi. Mbiu ya tamasha kwa mwaka huu ina angaz matakwa ya watu wa kisiwa hiki ya amani na muafaka.

Filamu ya ufunguzi, ni filamu yenye tunzo inayo muhusu mwanamziki maarufu Youssou N’Dour, I Bring What I love (Naleta nachokipenda), inayozungumzia ]addresses the themes of religious tolerance, harmony and peace.

 
Key Facts & Figures in 2009


• Waudhuriaji Mji Mkongwe: 45,000


• Waudhuriaji Dar es salaam: 200,000


• Wageni toka nje: 12,000


• Nchi zilizo shiriki: 43


• Filamu zitakazoonyeshwa mwaka huu: 100









Vitu Vya Kutazamia Mwaka Huu…


Fainali ya Kombe la dunia! Kwa kuzindua tamasha 2010 tutaonyesha mechi ya fainali ya kombe la dunia ndani ya Ngome Kongwe.






Filamu ya ufunguzi

 
Youssou N’Dour. I Bring What I Love Ni filamu yenye tunzo nyingi. Ya kuhamasisha, inayotupeleka kwenye safari ya kimziki, yenye ushuhuda wa nguvu ya sauti ya mtu mmoja kuhamasisha mamilioni. Muongozaji wa Filamu: Elizabeth Chai Vasarhelyi. Imedhaminiwa na SIGNIS.

 
Nipe Jibu: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza . Filamu ya kwanza ya kuchanganya Muziki na kuigiza Muongozaji Nadine Louise Fasera. Nipe Jibu ni filamu nzuri ya Kiswahili yenye kuchanganya muziki iliyotengenezwa kwa mtazamo wa kisasa na kitamaduni kwa simulizi iliyochangamka juu ya binti yatima anayeishi kwenye maisha ya ndoto.

 
My Policy: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Kijana mdogo mfanya biashara anapigwa risasi kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa anarejea nyumbani kwake akitokea kwenye tafrija yake kusherehekea siku hii muhimu akiwa na mchumba wake, Victoria.






Wiki chache baadae, Yule aliyempiga risasi amjia na kumchoma kisu hadi kufa. Kwa kupagawa na pigo hili, Victoria aamua kuhama Montreal na kuanza maisha mapya, Lakini muuaji amjia nay eye pia.... Muongozaji: Phad Mutumba

Motherland: African premiere - Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Africa

Ana’s Playground: African premiere

Lamu’s Maulid: world premiere

Inside Life: world premiere


Pumzi: East Africa’s first ever science fiction film


A sneak preview of Twiga Stars










Filamu za Watoto!

 
Kwa kushirikiana na taasisi ya filamu ya Kidanish, Maonyesho ya filamu za Watoto zitaonyeshwa makundi makubwa ya Watoto, zikiwa zimetafsiriwa kwa Kiswahili kwajili ya Watoto na vijana wa Mji mkongwe.



Art exhibitions
 "Hopes in Harmony" (Matumaini yenye Kuafikiana) – Onyesho la picha yanayoletwa na mpiga picha toka Italy, Carlo Deste


"Colour Bash" – Uchoraji wa vitenge kutoka pande mbalimbali za Afrika, na Mahelia de Randamie


Artwork kutoka wakina mama wa Iranian



Hii inaletwa na Ubalozi wa Iranian embassy


kwa kushirikiana na Soko Filam, ambapo watengeneza filamu na wachongaji toka Zanzibar wanakuja kuonyesha na kuuza bidhaa zao..

Tasnia

ZIFF ni tukio muimu kwenye jumuiya ya Cinema duniani. Festival Forum na Festival of Festival program inatoa nafasi kwa wasambazaji, mapromota, waongozaji wa filamu na waandaji kukutana ili kukomaza mizizi kwenye tasnia ya filamu kwenye nchi zinazoendelea.

 
Mwaka huu wawakilishi toka Trinidad na Tobago, Uganda, Holland, Iran, Mexico and Italy watashiriki ZIFF kujadili nafasi ya matamasha ya filamu kwenye nchi zinazoendelea.
 Warsha

ZIFF itaendesha warsha tatu wakitoa upendeleo kwa ushiriki wa waandaji filamu toka ukanda huu wa Afrika mashariki kwa waandaji wenye kuonyesha hari na vipaji vyenye mlengo wa kuibuka kwenye tasnia hii.

 
WARSHA ZA NAMNA YA KUOMBA MISAADA YA KIFEDHA KUANDAA FILAMU NA WARSHA – warsha itaongozwa na wakufunzi toka Sweden and Uganda

UANDAAJI WA MAKALA: CONNIE FIELD – Warsha hii ya siku nzima italeta mtazamo mzima wa namna ya kuandaa makala chini ya usimamizi wa mshikiliaji wa tunzo ya uandaaji wa makala(producer / director), Connie Field.
CINEPHILMS:UTENGENEZAJI WA FILAMU KUTUMIA SIMU YA MKONONI – Hii warsha ya aina yake itaongozwa na Jonathan Dockney wa chuo kikuu cha Natal South Africa. Utengenezaji wa filamu kwa kutumia simu za mkononi ni teknolojia inayo ibuka kwa kasi sana. Njo ujifunze jinsi ya kutengeneza filamu kwa simu!


 Kwa maelezo zaidi : www.ziff.or.tz


au ; www.ziff.or.tz/press. Pia unaweza kuwasiliana na Asmah Makua


(Swahili Press) asmahmakau@yahoo.co.in/ Tel no: 0713711413






Laura Martin-Robinson


(English language Press)


press@ziff.or.tz






Tel: +255 782689845

No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)