Wednesday, June 9, 2010



    ATANGAZA  NIA   YA   KUGOMBEA  UBUNGE   KWA  TIKETI   YA    CHADEMA  JIMBO  LA  NZEGA.

 


BWANA  John  Massanja  Mezza  amejiunga  na chama cha Chadema  na kutangaza azima  yake  ya kugombea  ubunge  kupia  chama  cha chadema  jimboni  Nzega  akitokea  chama cha  T L P.


      Tukio  hilo limefanyika  juma pili  mwishoni  mwa  wiki jana  majira  ya   saa tisa  arasiri   katika   viwanja  vya  parking  mjini  Nzega.Mezza  amefikia  uamuzi huo wa  kujiunga  na chadema  baada  ya  kuona  vyama  vingine  havina  maadili wala  muelekeo  mzuri  wa kisiasa na kufikia  uamuzi huo.


     Wananchi  wakionekana  kumuunga mkono  Bwana  John  Massanja  Mezza  kwa kuitikia  kwa wingi kujionea  kwa tukio hilo jinsi lilivyo fanyika.


     Akizungumza na  wananchi  Mezza  alisema  ameamua kujiunga  na chama hichi ilikutetea  wananchi  wa Nzega,kwa  kipindi  kilefu kukosa  muwakilishi  wa kweri ndani ya  Bunge.na kwa  kipindi  kilefu kukosa chama  chenye muelekeo  mzuri wa kisiasa  na kuamua kujiunga  na chama   cha  Demokrasia.


     ''Nawa hakikishia  wana Nzega kazi ipo,kazi imeanza kazi ipo  hakuna kulala  mpaka  kieleweke,hiyo ndiyo salam yangu  mkawaeleze  wana CCM''.alisema  Mezza  kwa  sauti kubwa  mbele ya umati wa  watu.kauri hiyo  iliufanya  umati  huo  kusisi mua  nawengine  kujiuliza  maswari  mengi yasiyo pata  majibu.


    Mratibu  wa Vijana Mkoa wa Kigoma  bwana  Yunusi  Rashidi Ruomvya amempongeza  bwana  Mezza kujiunga na  chama  cha Demokrasia  na kuachana na vyama  visivyokuwa na  muelekeo.amewataka   viongozi  wa chama wilaya  kumpa ushirikiano mzuri katika  kutetea  haki katika  jamii.

     Akitoa  mifano mbali  mbali bwana  Yususi  alisema  mabadiliko  ya  Kigoma  ya fanyike  na Nzega. amewataka  wananchi  wa Nzega  kuwa  na  mabadiliko  katika  chaguzi  zijazo   ilikuleta   changamoto   wilayani   na  mpaka  Bungeni kwa  ujumla.

     Katika  hatua  nyingine Bwana Yunusi  amewataka   wananchi   hao  kuzingatia  kanuni  za uchaguzi   hasa  kuongopa  kununuliwa  kwa njia  ya  vitu  vidoviudogo,akitoa mifano  ya  kanga,kofia na  Tshert.amewa  sisitiza  kuogopa  rushwa  katika  kipindi  hiki  na kijacho cha   cha uchaguzi.


      Katibu   Mkoa wa Kigoma Chadema  bwana  Msafiri  wa  Marwa  akitoa salam  zake  kwa  wananchi hao.amewataka   kuwa  na moyo  wa ujasiri  juu  ya maamuzi yao hasa  kwa  mambo ya  maendeleo.


     ''Wananchi  wa Nzega  nawaomba muwe  na maamuzi ya busara  hasa  kwa siku chache  pale  Bunge  litakapo  fungwa.tuchanguwe   mtu  anaye afaa,mwenye  uwezo  wakuongoza , msichague  chama ,kabila  wala rangi kwani  hata  hivyo  majuto  mmeyaona''alisema  bwana  Marwa.


       ''kwa sasa  tumefurahi  wamejitokeza  watu wenye  uwezo mzuri  wakututetea  kwani hatuna  mwakilishi ambaye anatusaidia,tunamuomba  mzee huyu  aongeze  ujasiri tupo bega  kwa bega''alisema  mkazi huyo hakutaka  jina lake litajwe.

     

       




No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa