ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA JIMBO LA NZEGA.
BWANA John Massanja Mezza amejiunga na chama cha Chadema na kutangaza azima yake ya kugombea ubunge kupia chama cha chadema jimboni Nzega akitokea chama cha T L P.
Tukio hilo limefanyika juma pili mwishoni mwa wiki jana majira ya saa tisa arasiri katika viwanja vya parking mjini Nzega.Mezza amefikia uamuzi huo wa kujiunga na chadema baada ya kuona vyama vingine havina maadili wala muelekeo mzuri wa kisiasa na kufikia uamuzi huo.
Wananchi wakionekana kumuunga mkono Bwana John Massanja Mezza kwa kuitikia kwa wingi kujionea kwa tukio hilo jinsi lilivyo fanyika.
Akizungumza na wananchi Mezza alisema ameamua kujiunga na chama hichi ilikutetea wananchi wa Nzega,kwa kipindi kilefu kukosa muwakilishi wa kweri ndani ya Bunge.na kwa kipindi kilefu kukosa chama chenye muelekeo mzuri wa kisiasa na kuamua kujiunga na chama cha Demokrasia.
''Nawa hakikishia wana Nzega kazi ipo,kazi imeanza kazi ipo hakuna kulala mpaka kieleweke,hiyo ndiyo salam yangu mkawaeleze wana CCM''.alisema Mezza kwa sauti kubwa mbele ya umati wa watu.kauri hiyo iliufanya umati huo kusisi mua nawengine kujiuliza maswari mengi yasiyo pata majibu.
Mratibu wa Vijana Mkoa wa Kigoma bwana Yunusi Rashidi Ruomvya amempongeza bwana Mezza kujiunga na chama cha Demokrasia na kuachana na vyama visivyokuwa na muelekeo.amewataka viongozi wa chama wilaya kumpa ushirikiano mzuri katika kutetea haki katika jamii.
Akitoa mifano mbali mbali bwana Yususi alisema mabadiliko ya Kigoma ya fanyike na Nzega. amewataka wananchi wa Nzega kuwa na mabadiliko katika chaguzi zijazo ilikuleta changamoto wilayani na mpaka Bungeni kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Bwana Yunusi amewataka wananchi hao kuzingatia kanuni za uchaguzi hasa kuongopa kununuliwa kwa njia ya vitu vidoviudogo,akitoa mifano ya kanga,kofia na Tshert.amewa sisitiza kuogopa rushwa katika kipindi hiki na kijacho cha cha uchaguzi.
Katibu Mkoa wa Kigoma Chadema bwana Msafiri wa Marwa akitoa salam zake kwa wananchi hao.amewataka kuwa na moyo wa ujasiri juu ya maamuzi yao hasa kwa mambo ya maendeleo.
''Wananchi wa Nzega nawaomba muwe na maamuzi ya busara hasa kwa siku chache pale Bunge litakapo fungwa.tuchanguwe mtu anaye afaa,mwenye uwezo wakuongoza , msichague chama ,kabila wala rangi kwani hata hivyo majuto mmeyaona''alisema bwana Marwa.
''kwa sasa tumefurahi wamejitokeza watu wenye uwezo mzuri wakututetea kwani hatuna mwakilishi ambaye anatusaidia,tunamuomba mzee huyu aongeze ujasiri tupo bega kwa bega''alisema mkazi huyo hakutaka jina lake litajwe.
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa