ASLIMIA 60 YA WATANZANIA HAWAPATI HUDUMA ZA KIBENKI-KIKWETE
RAIS Jakaya Kikwete,amesema kuwa,usalama wa fedha nyingi za watanzania upo mashakani kutokana na wengi wao kuzihifadhi majumbani ambako si pahala salama. Kikwete alitoa kauli hiyo jana jioni mjini Moshi katika uzinduzi wa tawi la Benki ya Biashara ya Kenya(KCB) tawi la Tanzania ambalo ni tawi la 11 kwa hapa nchini katika siku yake ya pili ya ziara ya siku mbili mkoani Kilimanjaro.
Alisema hatua ya watanzania wengi kuweka pesa zao majumbani inatokana na kutofikiwa na huduma za kibenki na kutoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuweka pesa zao benki alikodai ni pahala salama . Alitoa wito kwa mabenki kuanza kutoa elimu kwa wananchi ili wajenga utamaduni wa kuweka pesa zao benki na kuwaeleza faida ambazo watazipata ikiwamo usalama wa pesa zao na ukopeshwaji wa mikopo.
Hata hivyo,Rais Kikwete aliendeleza kilio chake kwa mabenki juu ya ukubwa wa riba ambazo aliidai kuwa ni kikwazo kikubwa kwa wateja na wafanyabiashara kukopa na kuyataka mabenki hayo kuona umhimu wa kupunguza riba hizo.
Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo hapa nchini,Edmund Mndolwa,alisema katika taarifa yake kwa Rais kuwa,hadi sasa benki hiyo inaomtaji wa Dola za Kimarekani Bilioni 2.6 huku ikiwa na matawi katika nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Sudan ya kusini.
Alisema k uwa,Benki hiyo imeweza kuwa na wateja wapatao 170,000 katika nchi hizo wanachama wa EAC yalipo matawi yake huku ikiwa na matawi katika mikoa ya Dar es salaam,Zanzibar,Morogoro,Arusha,Kilimanjaro na Mwanza.
|
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa