Translate in your language

Tuesday, May 25, 2010

 

 

 

MWANAFUNZI WA MAKUMIRA AIBA GARI AGONGA MTI NA KUFA

 

 

Hai

 

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Makumira

iliyopo Mkoani Arusha, amefariki dunia  papo hapo , baada ya gari

alilokuwa ameiba kugonga mti katika maeneo ya Kia Wilayani hai  akiwa

katika harakati za kutoroka

 

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa Habari Kaimu Kamanda wa Polisi

Mkoani Kilimanjaro Hilda Kinabo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May

23,majira ya saa 9:00 asubui katika eneo la Community House karibu na

uwanja wa ndege wa Kia.

 

Kamada alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Skadi Athumani (21)ambaye

alifika nyumbani kwa Albart Mgambilo na kukuta gari hilo likiwa

limeegeshwa na ndipo alipotumia funguo za bandia na kufanikwa kuondoka

nalo.

 

Kinabo alisema kuwa baada ya mwanafunzi huyo kufanikiwa kuondoka na

gari hilo,kama umbali wa kilimita 2 katika eneo la shule ya msingi ya

Asunta aligomga mti na kufariki dunia.

 

Hata hivyo Kamanda alisema kuwa mmiliki wa gari hilo alipewa taarifa

na baadhi ya majirani walioshuhudia ajali hiyo, huku wakidhani kuwa

mmiliki wa gari hilo ndiye aliyepata ajali lakini walipoangalia kwenye

gari ndipo walipomkuta mwanafunzi huyo.

 

Matukio ya wanafunzi kujiingiza katika wizi wa magari pamoja na

uporaji yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara ambapo Kaimu Kamanda

amewataka waalimu kutoa elimu kwa wanafunzi juu ya adhari ambazo

zinatokana na wanafunzi kujiingiza katika vitendo vya ujambazi.


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)