WAPIGA kura wa jimbo la Njombe Magharibi wamemchagia kiasi cha shilingi 20,000 mbunge wa jimbo hilo Yono Kevella ili muda ukifika achuku fomu ya kugombea tena ubunge katika jimbo hilo na kumtaka aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Thomas Nyimbo kutafuta shughuli nyingine ya kufanya na sio kurudia kugombea ubunge kwani kufanya hivyo ni sawa na kula matapishi yao. Wananchi hao wa kijiji cha Mlevela kata ya Igima walitoa msimamo wao huo juzi katika harambee iliyoendeshwa na mbunge Kevella ambapo pia mbali ya kuanchagi fedha hizo za kuchukua fomu pia walimuunga mkono katika harambee hiyo kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 1 zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo. Akizungumza baada ya kumalizika kwa harambee hiyo kwa niaba ya wakazi wa kijiji mwenyekiti wa chama cha TLP jimbo la Njombe Magharibi Yohana Mgowelo alisema kuwa toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 kijiji hicho hakijapata kuwa na kituo cha afya hali iliyokuwa ikiwalazimu wagonjwa kutembea masaa zaidi ya mawili kwenda kupata huduma ya afya katika kijiji cha jirani ama katika hospitali ya wilaya ya Njombe. "Mimi hapa ni mwenyekiti wa jimbo hili la Njombe Magharibi kupitia chama cha TLP ….ila ukweli lengo letu wapinzani sio kubeza kila jambo ….jimbo hilo huyu ni mbunge wa pili kuongoza ambapo mtangulizi wake alikuwa Thomas Nyimbo …lakini maendeleo yaliyopatikana sasa huwezi linganisha nay ale ya Nyimbo ….sasa kwanini tusimpongeze hata kwa kutuwezesha kupata huduma hii ya afya hapa…nasema tupo pamoja"alisema kiongozi huyo Pia alihoji sababu za wabunge wa CCM ambao wamepata kuongoza majimbo na kung'olewa katika nafasi zao kurudi kutaka kugombea tena ubunge na kuwa ni vema wananachi kuwa makini na njama chafu zinazofanywa na chama cha mapinduzi kwa kuendelea kuwapitisha wabunge wale wale miaka yote. Hata hivyo kwa upande wake mbunge Kevella akiwapongeza wananchi hao kuwa michango yao kwa ajili ya shuguli za kimaendeleo alisema kuwa jimbo hilo ni moja kati ya majimbo yanayo piga hatua kubwa katika maendeleo na kuwa mbali ya Manispaa ya Iringa kuwa na idadi kubwa ya vyuo vikuu ila bado wilaya ya Njombe katika jimbo la Njombe Magharibi ni miongoni mwa wilaya na majimbo yenye maendeleo makubwa kwa kuanzisha chuo kikuu kishiriki cha Tumaini . Kevella alisema kuwa pamoja na kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Thomas Nyimbo ameweza kuponda jitihada za kimaendeleo katika jimbo hilo ila bado wananchi wana kila sababu ya kuwabeza wale wote hasa wana CCM wanaotaka kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ambao wanajitokeza kupinga kazi zilizofanywa na chama hicho . Kwani alisema ni vizuri kazi ya kupinga ifanywe na wapinzani ila sio wana CCM na kuwa mwana CCM mwenye tabia kama ya Nyimbo ya kupinga kazi zilizofanywa na chama tawala chini ya Rais Jakaya kikwete atakuwa amepoteza mwelekeo wa kuja kuomba kuwatumikia wananchi . Mbunge huyo alisema kuwa kutokana na kituo hicho cha afya kukamilika bila kuwa na kitanda hata kimoja kwa upande wake kama mbunge atajitolea vitanda vyote katika kituo hicho pamoja na kununua madawati katika shule ya awali ya kijiji cha Idunda ambayo wanafunzi wake zaidi ya 60 pamoja na walimu wamekuwa wakikaa chini. Wakati huo huo wana CCM katika kata hiyo wamekitaka chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe kukemea tabia ya uongo kwa wanachama wanaotaka kuwania ubunge katika jimbo hilo ambao wamekuwa wakiwasema uongo wabunge na madiwani wa CCM huku wakisahau kuwa kauli zao na uongo zinakiweka pabaya chama hicho na kuonekana vibaya kwa wapinzani kuwa hakuna jipya ambalo limefanywa kwa kipindi chote cha miaka mitano alisema katibu wa CCM kitongoji cha Idunda Ayubu Mwipela
|
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa