Translate in your language

Sunday, May 16, 2010

 

KICHANGA CHA SIKU 25 CHATEKETEA KATIKA MOTO

 

Na Mwanablog wetu Dar

 

 

WATOTO  wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam likiwemo la kichanga kilichokuwa na siku 25 kuteketea na moto.

 

Katika tukio la kuteketea kwa kichanga hicho, jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Msime aliwaambia waandishi wa Habari  kuwa ajali hiyo ilitokea  majira ya saa moja na nusu usiku  huko maeneo ya Ferry Kigamboni baada ya moto kuzuka ghafla kwenye nyumba iliyokuwa na vyumba sita na kuteketeza chumba hicho kimoja alichokuwa kichanga huyo.

 

Kamanda Msime alieleza kuwa,chumba hicho kilikuwa cha mpangaji ambaye ni mama wa kichanga hicho, Mwantoro Haji (30), ambaye aliwasha kibatari na kutoka kuteka maji nje ya nyumba hiyo., ambapo moto huo ulizuka ndani ya chumba hicho na kuteketeza kila kitu pamoja na kifo cha kichanga hicho kilichokuwa na siku 25 ambaye jina lake ni Zainab Abdala.

 

Moto  huo ulizimwa kwa juhudi za wananchi wa eneo hilo na upelelezi unaendelea.

 

Katika tukio jingine, Kamanda wa Polisi MKoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alisema kuwa, mtoto David  Jeras (7) alikufa maji baada ya kutumbukia katika mtu Mbezi.

 

Kalinga alieleza kuwa, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la Saba wa shule ya msingi Londa, alikwenda mtoni hapo na wenzake kuvua samaki, ghafla aliteleza na kunywa maji mengi yaliyopelekea kifo chake.

 

Mahiti ya mtoto huyo iliopolewa na wananchi na imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.

 

 

 


No comments :

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa

Kijiweni (nipe 5)