Wavuvi 77 watekwa nyara katika bahari Hindi ![]() | ||||
Msemaji wa kikosi cha Muungano wa Ulaya kinachopambana na uharamia, amesema maharamia wa Kisomali, wameandikisha rekodi kwa kuwateka nyara idadi kubwa ya mabaharia kwa wakati mmoja, katika bahari ya Hindi. Amesema tukio hilo lilitokea nje ya eneo linalothibitiwa na wanajeshi wa kimataifa. Duru zinasema wavuvi sabini na saba walitekwa nyara baada ya mashua tatu za uvuvi kutekwa takriban kilomita elfu mbili kutoka ufuo wa Somalia. Shambulio hilo ndilo la kwanza kuwahi kutekelezwa na maharamia hao katika eneo hilo la bahari katika kipindi cha miaka miwili na msemaji huyo amesema ni ishara ya mafanikio ya doria inayodumishwa na wanajeshi wa kimataifa. |
No comments :
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa